Home » » OFISA MTENDAJI KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA

OFISA MTENDAJI KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA



TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru)wilayani Serengeti mkoa wa Mara  imemfikisha mahakamani afisa mtendaji wa kata ya Machochwe Peter Hagare kwa shitaka la kuomba na kupokea rushwa ya sh.100,000.

Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Serengeti Amon Kahimba  Mwanasheria wa Takukuru Erick Kiwiya amesema kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo aprili 10 mwaka huu.
Kiwiya ameiambia mahakama hiyo kuwa siku  ya tukio mshitakiwa akiwa ni afisa mtendaji wa kata ya Machochwe, alimshawishi Mwita Buruna ampe fedha hizo ili ampe barua ya kumtambulisha mahakamani kwa ajili ya kumdhamini ndugu yake aliyekamatwa kwa kosa la kuingia hifadhini bila kibali.

Na kuwa Takukuru walipokea malalamiko kutoka kwa Buruno ya kudaiwa kiasi hicho cha fedha na kufuatilia kijijini na kufanya uchunguzi kwa wananchi na kubainika alipokea fedha hizo.

Mwanasheria huyo wa Takukuru amewataja waliotakiwa kudhaminiwa na Buruna kuwa ni Ghati Buruna na John Mogendi wakazi wa kijiji cha machochwe wilayani hapa.

Mshitakiwa amekana  shitaka na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti mawili yaliyotolewa na mahakama hiyo.

Sharti kwanza amemtaka mshitakiwa kujidhamini mwenyewe kwa sh.500,000 za maandishi na sharti la pili ni kuwa na watu wawili wanaoaminika wajidhamini kwa maandishi kila mmoja sh,mil.2. Kesi hiyo imepangwa kutajwa tena julai 27 mwaka huu.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa