ZAIDI ya kaya mia nne katika kijiji cha Weigita kata
ya Kibasuka Wilayani Tarime Mkoani Mara huwenda zikakumbwa na njaa kali
baada ya mashamba yao ya mazao zaidi ya hekali elfu tano kupelekwa na
maji baada ya Mto Mara kujaa maji na kuhama mkondo wake ambapo maji hayo
yamefika hadi mashambani na kwenye makaza ya wananchi huku mifugo 40 ikidaiwa
kufa mtoni wakati ikitoka malishoni.
Mwenyekiti wa kijiji cha Weigita
amesema kuwa Mafuriko hayo ya maji Mto Mara yanadaiwa kutokea
jana majira ya jioni ambapo ng'mbe 40 kutoka familia 3 zimepelekwa na
maji wakati ikivuka mto ikitokea malishoni na kwamba endapo jitihada za haraka
hazitafanyika kutatokea maafa makubwa kutokana na Mto kuendelea kumwaga maji.
Pia zaidi ya vijiji vitano
vilivyoko kando kando ya mto mara ambao ulima mazao kando kando mwa Mto
mara mazao yameweza kuharibiwa kutokana na mto mara kujaa na kuhama
mkondo ambapo baadhi ya wakazi wa natoka katika vijiji vya Gibaso,Kerende,Murito,Nyarero,Matongo,
.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime John
Henjewele amewataka wananchi kuacha kulima mazao katika maeneo ambayo si salama
ambayo yamekuwa yakitokea mafuriko ya maji ya mara kwa mara nakwamba watu
wanapaswa kuhama katika maeneo ambayo si salama kwa madai kuwa swala la
utatuzi wa Mto mara ni gumu na ni la kitaalamu zaidi na linahitaji pesa
nyingi.
0 comments:
Post a Comment