CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kinadaiwa kufanya mchezo mchafu dhidi ya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilaya ya Tarime katika
uchaguzi wa kuongoza Halmashauri ya Mji mpya wa Tarime. Mchezo huo
mchafu unadaiwa kufanywa na CCM, kutokana na hatua yao ya kutaka
kubadili hati ya kuunda halmashauri ya mji huo ambapo madiwani wa CCM
wanadaiwa kuandaa mkakati wa kumzuia diwani wa viti maalum wa Chadema,
ili asiweze kupiga kura.
Akizungumza na MTANZANIA kuhusiana na sakata hilo, Diwani wa Kata ya Sabasaba, Christopher Chomete (Chadema), alisema CCM inataka kutumia nguvu ili iweze kuongoza halmashauri hiyo kwa kuvunja taratibu zilizotolewa na TAMISEMI.
Diwani Chomete alisema, kitendo cha CCM kutaka kutumia nguvu ni kinyume cha sheria ya TAMISEMI namba 1 hadi 3, ambayo imeweka wazi namna ya upatikanaji wa viti maalumu.
Alisema kwamba, kutokana na hali hiyo, CCM Wilaya ya Tarime, inapinga hatua ya diwani wa viti maalum wa Chadema kuwa mjumbe wa kupiga kura kwa madai kuwa anaishi nje ya Mji wa Tarime.
“Chadema ina nafasi kubwa ya kuongoza Halamashauri ya Mji mpya wa Tarime, kutokana na kuwa na madiwani sita wakati CCM inao wawili.
“Kati ya hao madiwani sita wa Chadema, kati yao mmoja ni wa viti maalum, lakini CCM wamekuwa wanajenga hoja kuwa diwani wetu wa viti maalumu si mkazi wa mjini.
“Hata hivyo, hivi sasa CCM wanaendelea na mikakati yao ya kutaka kuwaleta madiwani watatu wa viti maalum ili waweze kupiga kura katika Halmashauri ya Mji wa Tarime kama njia ya kutaka kuiongoza halmashauri kwa nguvu,” alisema Diwani Chomete.
Alisema pia kwamba, kama CCM wataendelea na mkakati wao huo, Chadema wataangalia namna ya kwenda mahakamani kusimamisha uchaguzi huo ili wananchi wajue kuwa CCM ndio inakwamisha maendeleo yao.
“Muongozo wa TAMISEMI upo wazi katika uundwaji wa halmashauri ambapo Chadema hadi sasa ina madiwani watano, huku CCM ikiwa na wanne wakiwamo Mbunge wa Tarime, Nyambari Nyangwine na Mbunge wa Viti Maalum, Gaudentia Kabaka.
“Katika sakata hili, CCM inamuondoa Diwani wa Chadema wa Viti Maalumu na kutaka kuingiza madiwani wao na wabunge, sisi hatutaki na tutalipeleka suala hili kwa wananchi ili watuamulie.
“Pamoja na hayo, ni kwamba wakati Mkuu wa Mkoa wa Mara, Gabriel Tupa, anahutubia sherehe za Serikali za Mitaa wilayani Tarime, alisema tayari hati ya mji mpya wa Tarime anayo ofisini kwake na inaeleza utaratibu wa kuundwa kwa halmashauri, ambapo madiwani wa Chadema wapo wanne dhidi ya wawili wa CCM,” alisema.
Kwa mujibu wa diwani huyo, Chadema inaongoza Kata za Sabasaba, Nyamisangura, Turwa na Nyandoto huku CCM ikiongoza Kata za Bomani na Kitare.
Kwa upande wake, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, alisema hati ya mwanzoni iliyotolewa na TAMISEMI ilikuwa ikiwapa nafasi kubwa Chadema kuongoza halmashauri hiyo.
Kabaka aliyasema hayo wakati alipokuwa akitoa taarifa yake mbele ya kikao cha Halmashauri ya Mkoa wa Mara ambapo aliweka wazi namna sakata hilo linavyoweza kuleta vurugu za kisiasa wilayani humo.
“Hati ya awali ya TAMISEMI iliwatoa wabunge na madiwani wa viti maalumu kupiga kura wakati wa kumchagua mwenyekiti wa halmashauri na ni wazi inawapa nafasi Chadema kuongoza halmashauri,” alisema Waziri Kabaka.
Kutokana na hali hiyo, alisema iliamuliwa ufanyike uamuzi wa haraka ili kuweza kufuatilia suala hilo kwa kwenda kumuona Waziri wa TAMISEMI, Hawa Ghasia ili kufanya mabadiliko ya haraka na kuwaruhusu wabunge na madiwani wa viti maalum nao waweze kupiga kura.
Waziri Kabaka, alisema kuwa CCM Wilaya ya Tarime iliamua kumpa Nyangwine, jukumu la kufuatilia jambo hilo kwa karibu ili kuweza kubadili hati hiyo.
“Nadhani ndugu wajumbe hapa hamumuoni Mheshimiwa Nyangwine humu ukumbini, yupo kwenye majukumu muhimu kuhakikisha hati inabadilika na wabunge pamoja na madiwani wa viti maalumu wanapiga kura na CCM iweze kuongoza halmashauri ya Mji mpya wa Tarime.
“Nimewasiliana na Mheshimiwa Nyangwine ameniambia tayari kila kitu kimekamilika, baada ya kuonana na Waziri Ghasia na hati imebadilika sasa wabunge na madiwani wote wa viti maalum watapiga kura na hivyo CCM itaiongoza Halmashauri ya Mji mpya wa Tarime,” alisema Waziri Kabaka.

CHANZO GAZETI LA MTANZANIA
0 comments:
Post a Comment