Home » » MADIWANI WAWAKABA KOO DC, DED RORYA

MADIWANI WAWAKABA KOO DC, DED RORYA

MADIWANI wanaojiita kundi la okoa Rorya  lenye muungano wa baadhi ya Madiwani wa Chama cha CCM na Vyama vya wapinzani wamesema kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya Elias Goroi ni Kiongozi mchapa kazi hivyo wanaotaka ahamishwe wana njama ya kurudisha nyuma maendeleo Rorya.

Madiwani  hao waliokutana jana viwanja vya halmashauri ya Wilaya ya Rorya wamesema kuwa wanasikitika kwa kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha CCM Wilaya ya Rorya Samwel Keboye (namba tatu) kwenye vyombovya habari kudai kuwa wananchi na Madiwani wameandamana kutaka Dc  Goroi ahamishwe.

Madiwani wamekanusha  kuwa hakuna maandamano ya wananchi wala Madiwani yaliyofanyika nakwamba Dc Goroi na Mkurugenzi wa halmashauri Ephraem Ole Nguyaine hawapaswi kuhamishwa kwakuwa wamesaidia kuwawajibisha watumishi wabovu wanaojihusisha na ubadhilifu wa mali za umma na kuimalisha utawala bora.


Pendo odelle Diwani wa Viti maalum Tarafa ya Nyancha (ccm)ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa na mjumbe halmashauri ya ccm Wilayani hapo amemtaka mweyekiti wa CCM Keboye  kutenda  haki kwa usawa na siyo  kuwa kibaraka  na kuegemea kutetea upande mmoja wa Mbunge  kwa masalahi yake binafsi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa