WACHIMBAJI
wadogowadogo wa dhahabu wawili wamekufa baada ya kufukiwa na kifusi wilayani
Bunda, mkoani Mara.
Mwenyewkiti
wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Bunda, Bw. Joshua Mirumbe jana
amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kusema kuwa tukio hilo lilitokea juzi
katika kijiji cha Kamkenga tarafa ya Serengeti wilayani hapa.
Ofisa
tarafa ya Serengeti Bw. Jastine Rukaka, amewataja watu hao kuwa ni pamoja
Pascal William, mkazi wa Kamkenga wilayani Bunda na mwingine aliyetambuliwa kwa
jina moja la Robert, mkazi wa Mugumu wilayani Serengeti.
Bw.
Rukaka amesema kuwa wakati watu hao wakiendelea kuchimba dhahabu, ghafula
kifusi kiliporomoka na kuwafunika na kwamba mwenzao wa tatu yeye alinusurika
kifo baada ya kufanikiwa kutoka nje ya shimo hilo.
Amesema
kuwa tayari miili ya wachimbaji hao iliondolewa ndani ya shimo hilo a
kutambuliwa na kwamba polisi walifika katika eneo la tukio na kushuhudia vifo
vya watu hao
0 comments:
Post a Comment