Home » » Diwani ataka wajumbe wa kamati ya ukimwi kupima afya zao

Diwani ataka wajumbe wa kamati ya ukimwi kupima afya zao

WAJUMBE wa kamati ya ukimwi, katika halmashauri ya wilaya ya Bunda, mkoani Mara, wameshauriwa kupima virusi vya ukimwi, ili aweze kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi katika suala zima la kuwahamasisha wananchi kupima afya zao na kuchukua tahadhali. Ushauri huo umetolewa jana na diwani wa kata ya Bunda Sitoo, BW. Sospeter Munubi (CCM), wakati akiachangia hoja kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Bunda, kilichofanyika katika ukumbwi wa halmashauri. Mhe. Munubi akichangia katika taarifa ya ukimwi iliyowasilishwa na mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Sospeter Masambu, ambaye pia ni makamo mwenyekiti wa halmashauri hiyo, alihoji kama wajumbe wa kamati hiyo wote wamekwishapima virusi vya ukimwi, kwani hawawezi kuhamasisha watu wengine kupima wakati wao wenyewe hawajapima. Mhe. Munubi alianza kwa kumshukuru rais Jakaya Kikwte, kwa kuwa mstari wa mbele katika vita juu ya ukimwi, na kusema kuwa katika kuonyesha mfano rais alipima afya yake na akawataka wajumbe wa kamati hiyo pia kuiga mfano huo. Amesema kuwa iwapo wajumbe wa kamati hiyo ya afya, elimu na maji, wakipima afya zao watakuwa mabalozi wazuri kwa kufikisha ujumbe kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha kuhusu kupima afya zao na kuchukuwa tahadhali, sanjari na kupewa ushauri nasaha. Akijibu hoja hiyo mwenyekiti wa halmashauri hiyo mhe. Joseph Malimbe, amesema kuwa suala la upimaji virusi vya ukimwi ni siri ya mtu, na kwamba lakini ni vema watu wote wakapima afya zao, kwani ukimwi hauchagui mjumbe wa kamati hiyo bali ni kwa watu wote na kwamba njia pekee ni kuacha ngono zembe ili kujiepusha na maambukizi ya ukimwi. Naye diwani wa kata ya Mcharo Julius Marigeri (CCM), ameshauri taarifa inayotolewa na kamati hiyo kwenye baraza hilo, iwe inaeleza bayana hali ya maambukizi katika wilaya na mkoa kwa ujumla yakoje, badala ya kuletwa kikao hicho bila kuwa na ufafanuzi huo. Bw. Marigeri amesema kuwa hali hiyo itawafanya madiwani kujua hali halisi na kufikisha taarifa hiyo kwa wananchi juu ya hali halisi ilivyo, ambapo watachukua tahadhari juu ya mambukizi yakiwemo mapya. Akitoa taarifa ya ukimwi wilayani hapa, Mganga mkuu wa wilaya ya Bunda, Dk. Rainer Kapinga, alisema kuwa maambukizi ki mkoa yameshuka kutoka asilimia 7.7 mwaka 2010 na kufikia asilimia 5.7, ambapo ki wilaya yameshuka kutoka asilimia 4.8 hadi asilimia 4.5.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa