Home » » CHAMA cha kuweka na kukopa (Mugumu hospitali)

CHAMA cha kuweka na kukopa (Mugumu hospitali)

Saccos,katika wilaya ya Serengeti mkoani Mara kimetumia zaidi ya sh,mil.700 kutoa mikopo  620 ya riba nafuu kwa wanachama wake 164  kwa kipindi cha 2008-2013.

Mhasibu wa Saccos hiyo,Daniel Mwambela ameiambia Redio Free Africa kuwamikopo hiyo  imeelekezwa kwenye shughuli za
Kilimo,ufugaji,biashara masomo kwa wanachama na familia zao, huku wanawake 87 wakichukua mikopo ikilinganishwa na wanaume 77.

Mhasibu huyo amesema licha ya wanawake kuwa wengi lakini wamekopa sh..361 ,761,987 na wanaume wakiwa wamekopeshwa sh. 400,514,500,na shilingi Mil. 3 zimetumika kuanzisha mradi wa m_pesa kama mtaji ili kusaidia watu wanao fika hospital kupata matibabu,na wanalipa kwa kipindi cha miezi mitatu hadi sitini.

Aidha Mwambera amesema Chama chao kimekopa katika benki ya Maendeleo vijijini(CRDB) kiasi cha sh.mil.438 kwa riba ya asilimia 16 na mpaka sasa wamefanikiwa kurejesha sh.312,907,420,na akiba waliyonayo kwa mjibu wa  taarifa  ya chama mpaka mwezi septemba mwaka huu ni sh.115,773,880,ikiwa ni hisa na mafungu ya wanachama.

Kuhusu changamoto zinazoikabili Saccos amesema ni ucheleweshaji wa urejeshaji mkopo kutoka kwa wanachama wake,sababu kubwa ikiwa ni kuchelewa kwa mishahara kwa watumishi wa hospitali hiyo iliyo chini ya kanisa la KMT,pia riba kubwa zinazotozwa na taasisi za fedha hapa nchini

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa