Musoma.Wananchi wa Tarafa ya Nyanja, wilayani
Butiama, wametakiwa kulima kilimo chenye tija kwa faida ya familia zao
na taifa kwa jumla badala ya kuendekeza kilimo cha mazoea.
Rai hiyo ilitolewa juzi na Meneja wa Maendeleo ya
Biashara na Usafirishaji katika Kiwanda cha Mbolea ya Minjingu Arusha,
Julius Nyabicha wakati akitoa elimu ya kilimo chenye tija.
Nyabicha alisema kama wananchi watakubali
kubadilika na kulima kilimo chenye tija kwa kuwekeza katika kilimo,
wanaweza kuiepuka njaa ya mara kwa mara na kutegemea chakula cha msaada.
Pia aliwataka wananchi kutambua kuwa kilimo ni ajira na biashara ya kimataifa na kwa msingi huo, lazima wawekeze zaidi.
Meneja huyo alisema ikiwa wananchi watakubali
kubadilika na kuanza kulima kilimo cha kisasa kinachoambatana na
matumizi ya mbegu bora na mbolea ya kupandia ya Minjingu wataondokana na
umaskini.
“Mkulima anatakiwa awe mwelewa sana, akubali
kuwekeza katika kilimo kwa kununua pembejeo za kilimo hata kama ni kwa
mkopo, bila kusubiri msaada wa Serikali,” alisema Mahemba.
Kwa upande wao, wakulima katika eneo hilo,
walielezea kufarijika kwao na mafunzo hayo ambayo walisema watayatumia
kikamilifu ili kuzalisha mazao bora kwa faida yao na taifa kwa jumla.
Waliahidi kutumia mbegu bora na mbolea za kupandia zote muhimu.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment