MKUU
wa Mkoa wa Mara John Tuppa amewataka waandishi wa habari na vyombo
vya habari nchini kuandika na kuripoti habariz a kweli za uhalisia
kwa kuzingatia maadili ili kuepusha migogoro kati ya
Serikali,Wanasiasa na jamii kwa ujumla.
RC
Tuppa amesema kuwa hivi karibuni iliripotiwa taarifa katika baadhi
ya vyombo vya habari kuwa Mbunge Rameck Airo akiwa kwenye mkutano wa
wananchi wa kijiji cha Bunganjo kata ya Bukwe alisema DC Goroi
anashiriki kwenye mtandao na wezi wa Ng’ombe ambapo Mbunge Airo
alikana kutamka kauli hiyo.
Mbunge
Airo amekana tuhuma hiyo jana mbele ya kikao cha wazee mashuhuri wa
Rorya wakiwamo viongozi wa dini kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa
wa Mara John Tuppa aliyeongozana na viongozi wa Mkoa na viongozi wa
chama cha CCM na kuwataka viongozi hao kusema tofauti zao
mbele yao ili kutafuta suluhu.
Hata
hivyo RC Tuppa amewapatanisha viongozi hao ambapo wote
walikubaliana kuachana na tofauti zao lakini kwa upande wa vyombo vya
habari DC Goroi amesema atavifikisha mahakamani vyombo vya
habari vilivyomkashifu kwakuwa Mbunge kakana kutotamka
kauli hiyo kwa kile alichosema imemvunjia heshima
kwa jamii.
0 comments:
Post a Comment