Home » » Mtoto wa miake minne apigwa na kulazimishwa kula kinyesi chake

Mtoto wa miake minne apigwa na kulazimishwa kula kinyesi chake

MWANAMKE mmoja amekamatwa na raia wema katika wilaya ya Bunda, mkoani Mara, na kupelekwa polisi baada ya kunyanyasa mtoto wa kambo wa miaka minne, kwa kumpiga na kumlisha kinyesi chake kwa madai kuwa amejisaidia ndani ya nyumba yake.

Mwanamke huyo Joyce Maneno, mkazi wa mtaa wa Idara ya maji katika mji wa Bunda, amekamatwa na wananchi wa eneo hilo, baada ya kugundua kunyanyaswa kwa mtoto huyo, kwa kumchapa, kumpiga, na kumlisha kinyesi chake.

Wakitoa maelezo na kuthibitibishwa na maafisa wa polisi wilayani hapa, wananchi hao wamesema kuwa mwanamke huyo amekuwa akifanya ukatili huo mara kwa mara, na kwamba anafanya hivyo wakati mume wake amekwenda visiwani kwenye shuhuli zake za uvuvi.

Afisa maendeleo ya jamii wa wilaya ya Bunda, Bi. Chiku Mshora, amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kuongeza kuwa baada ya mwanamke huyo kudhaminiwa polisi, alisikika akijigamba kuwa mtoto huyo atamfanyia jambo lolote lile, kwani hawezi kumwaribia maisha yake kwa mumewe.

Wakati huo huo, mtoto, mdogo aliyekuwa ameozwa kwa mwanaume wa miaka 54, amepelekwa kwenye kituo cha kulea watoto kiitwacho Jipe Moyo, kilichoko mjini Musoma, ili aweze kutunzwa huko na kusomeshwa shuleni.

Mtoto huyo alikuwa ameolewa na mzee huyo, baada ya kutoa kishika uchumba kiasi cha shilingi 55,000 kwa baba yake mzazi, ambapo sasa mzee huyo pamoja na baba,wako mahabusu baada ya kunyimwa dhamana na mahakama ya wilaya ya Bunda, kwa kushindwa masharti ya dhamana.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa