Musoma. Mkoa wa Mara umeanza kuchukua hatua mbalimbali za kupambana na ongezeko la vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga.
Mkakati huo unaambatana na kuanzisha mpango maalum wa ujenzi wa vituo vya afya ili kusogeza huduma kwa jamii.
Tayari ujenzi wa vituo 12 vya afya umeshakamilika
kupitia mpango huo. Hayo yalisemwa juzi katika kikao cha Kamati ya
Ushauri ya mkoa huo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara, Samson Winani,
alisema kutokuwepo kwa huduma karibu kuchangia vifo vingi vya wanawake
wajawazito na watoto.
Alisema kwa kuzingatia ukubwa wa tatizo hilo, mkoa umeamua kuboresha vituo vya afya vilivyopo ili sasa vitoe huduma bora.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment