WATU wanne wa familia moja wakiwamo watoto wawili, wamelazwa katika
Zahanati ya Kata ya Kisorya wilayani Bunda, baada ya kupoteza fahamu
katika mazingira ya kutatanisha wakiwa wamelala ndani ya nyumba yao.
Wanafamilia hao, Juma Abdalah na mkewe Hadasa Juma na watoto wao,
Adventina na Vaileth, walinusurika kifo baada ya wananchi kuvunja mlango
wa nyumba walimolala na kuwakimbiza katika zahanati hiyo kwa ajili ya
matibabu.
Diwani wa Kata ya Kisorya, Misana Jigwila na Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Mashaka Mahulilo, walisema tukio hilo ambalo limeripotiwa polisi, lilitokea jana saa moja asubuhi katika Kijiji cha Nambubi.
Ilielezwa kuwa wanafamilia hao walipoteza fahamu na kuishiwa nguvu wakiwa wamelala ndani ya nyumba hiyo na waligunduliwa na ndugu yao mmoja alipofika nyumbani hapo na kukuta mlango ukiwa umefungwa kwa ndani huku wao wakikoroma kwa sauti kubwa.
Kutokana na hali hiyo, wananchi pamoja na viongozi walifika katika eneo hilo na kuvunja mlango wa nyumba hiyo, ambapo waliwakuta wote wakiwa hawajitambui na kuwakimbiza kupata matibabu.
“Tulifika katika eneo hilo na kuvunja mlango na kuwakuta wote wakiwa hawajitambui na wameishiwa nguvu na ndipo tukawakimbiza katika zahanati ya kata. Sasa bado hatujajua nini kilichowasibu,” alisema Jigwila.
Mganga wa zamu katika zahanati hiyo, Dk. Stephen Mashaga, alisema hadi jana mchana walikuwa hawajajitambua na juhudi za kuokoa maisha yao zinafanyika ikiwa ni pamoja na kuchunguza kile kilichowasibu na kufikia hali hiyo.
Wakazi wa Kijiji cha Nambubi na Kata ya Kisorya kwa ujumla walilihusisha tukio hilo na mambo ya ushirikina.
Chanzo:Mtanzania

0 comments:
Post a Comment