WATU wawili wamefariki dunia na mwingine kujeruhiwa baada ya
kuporomoka na kuanguka ndani ya shimo la kuchimba dhahabu la Gokona la
mgodi wa dhahabu wa North Mara uliopo katika Kijiji cha Kewanja, Kata
ya Kemambo, wilayani Tarime, Mara.
Kaimu Kamanda wa Polisi Tarime na Rorya, Sweetbert Njewike, alisema
jana kuwa watu hao walikuwa wameingia kuchimba na kutafuta mawe ya
dhahabu.
Aliwataja watu hao kuwa ni Samwel Cheiro (29), mkazi wa Kijiji cha
Nyakunguru aliyefia hospitalini akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa
tumboni na Jeremeia Joashi (25), mkazi wa Nyakunguru aliyefia eneo la
tukio aliyekutwa na jeraha kisogoni.
Alimtaja aliyejeruhiwa katika tukio hilo ni Wesiko Gitando (25) mkazi wa Kijiji cha Magomna alijeruhiwa kwenye nyonga.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Nega Marco, aliliambia
Tanzania Daima kuwa wanajiandaa kuifanyia uchunguzi miili ya marehemu
hao na taarifa zitatolewa baadaye.
Hatua hiyo inakuja kutokana na kuwapo kwa madai kuwa Cheiro alipigwa
risasi na polisi walipokuwa wakiwatawanya baadhi ya vijana maarufu kama
‘Intruders’ walipogoma kutoka katika eneo la mgodi huo baada ya
kuuvamia na kutaka kuokota mawe ya dhahabu.
Pia inadaiwa Gitaro alijeruhiwa kwa risasi za moto alipotupiwa na
askari hao walipokuwa wamesimama na marehermu huyo katika eneo la
barabara.
Chanzo;Tanzania daima
0 comments:
Post a Comment