Home » » Wanaodaiwa washirika wa muuaji Tarime kortini

Wanaodaiwa washirika wa muuaji Tarime kortini

Watu  wanane wanaodaiwa kuwa washirika wa mtuhumiwa wa mauaji ya watu kadhaa wilayani Tarime, marehemu Charles Range Kichune, aliyefariki wakati akipatiwa matibabu ya pumu akiwa mikononi mwa polisi, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime wakikabiliwa na kesi ya mauaji.
Wanashitakiwa kwa mauaji ya watu wanane na unyang’anyi katika kata za Turwa , Kitare na Binagi.

Ilidaiwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Tarime, Adrian Kilimi, na Mwendesha Mashitaka, George Lutonjo, alidai kuwa watuhumiwa 10  baadhi yao waliokuwa washirika wa marehemu Kichune ni pamoja na  mwendesha pikipiki Marema Mweri Kibwabwa  aliyekuwa akimsafirisha marehemu  wakati wa matukio na kumtorosha hadi Musoma.

Wengine ni Elizabeth  Kitara Mwita, Mairo Chacha Kegoro, Joram Mwita Chacha,  Simion  Marwa Bisumwa, Kyoma Manghu Nyaseba, Chacha Mahegere Bugichere na Yohana Mgosi Kimom.

Lutonjo alidai kuwa watuhumiwa katika nyakati tofauti kuanzi Januari 26 hadi Januari 28 waliua watu tisa katika kata za Turwa , Binagi na Kitare na kuwaua  kwa kuwapiga risasi  Zakaria Mwita Marwa, Erick Lucas, David Misiwa Yomami, Samwel Matiko,,Robert Machumbe, Juma Nyaitara, Marwa Mwita na Juma Marwa.

Watuhumiwa wote hawakutakiwa kujibu lolote kwani mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.
CHANZO: NIPASHE
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa