DIWANI wa Nyamisangura, Thobias Ghati (CHADEMA), ameitaka
Halmashauri ya Mji wa Tarime, mkoani Mara kutatua kero ya ukosefu wa
eneo la kuzikia na kusababisha maiti zaidi ya moja kuzikwa katika
kaburi moja.
Ghati aliibua hoja hiyo katika kikao cha kawaida cha Baraza la
Madiwani kilichomalizika wiki iliyopita mjini hapa. Hoja hiyo iliungwa
mkono na madiwani wanzake.
Alisema alishuhudia wananchi wakichimba kaburi katika maeneo ya maziko, eneo la Ronsoti na kukuta wamezikwa watu wawili.
Alisema waombelezaji hao walibaini watu wawili walizikwa kaburi moja
baada ya kukuta mafuvu ya vichwa viwili vilivyokuwa katika eneo
walilochimba kaburi kwa ajili ya kumzika mtumishi mmoja wa halmashauri
ya mjini wa Tarime.
Ghati aliitaka halmashauri yake isaidie kupatikana eneo jingine kwa ajili ya maziko kutokana na eneo la Ronsoti kujaa.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Venance Mwamengo, alisema tayari kumepatikana eneo jingine.
Mwamengo alisema walifanikiwa kupata eneo la ardhi ya mkazi mmoja wa
mjini hapa lenye ukubwa wa ekari 30 anayehitaji kulipwa fidia ya sh
milioni 39.
Chanzo;Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment