WANAKIJIJI cha Kibara B, wilayani Bunda, Mara, wamedai halmashauri
ya wilaya hiyo kupitia kwa Idara ya Ardhi imemmilikisha ardhi mwekezaji
mwenye mashine za kusaga na kuchukua mapato ya kijiji hicho bila
ridhaa yao.
Wakiwakilishwa na mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho, Mafwili
Mnyaga, wananchi hao walitoa kero hiyo juzi kwa Mbunge wa Mwibara,
Kangi Lugola, aliyekuwa akihutubia mkutano wa hadhara kijijni hapo.
“Mbunge sisi wananchi wa Kijiji cha Kibara B tunasikitishwa na
kitendo cha Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, kupitia Idara ya Ardhi
kutupora ardhi yetu bila kutushirikisha na kuchukua mapato,” walisema
kwa nyakati tofauti.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment