Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Chanzo cha vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga
mkoani Mara ni utendaji kazi mbovu na kukosekana uadilifu, wauguzi
kukosa wito na upungufu wa wataalamu wa afya.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara,
JohnTuppa wakati akifungua kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa
mpango mkakati wa kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto
wachanga mkoani hapa kwa kipindi cha Julai 2013 hadi Januari 2014.
Tuppa alisema amekuwa akipokea malalamiko kutoka
kwa wananchi kuwa wauguzi na wataalamu wa afya wamekuwa wakichangia vifo
vya akina mama na watoto wachanga, kutokana na huduma wanazopata
kutowaridhisha.
Aidha mkuu huyo wa mkoa aliwataka wakuu wa wilaya
kufuatilia katika vituo vya afya, zahanati na hospitali za wilaya kwa
lengo la kuboresha huduma za afya na kuwataka wauguzi na wataalamu wa
afya kufanya kazi za uuguzi kama wito wao unavyowataka.
“Haiwezekani vifo vya akina mama wajawazito na
watoto wachanga vikaendelea kutokea kutokana na uzembe wa watu wachache
kushindwa kutoa huduma za afya zinazofaa. Atakayebainika, sheria na
taratibu za kinidhamu zitafuata dhidi yake,” alisema Tuppa.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment