Home » » WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUUA PUNDAMILIA

WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUUA PUNDAMILIA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399
WATU wawili wanaodaiwa kuwa wawindaji haramu sugu jana wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Bunda, mkoani Mara, wakikabiliwa na kosa la uwindaji haramu, baada ya kukamatwa wakiwa wameua mnyama mmoja aina ya Pundamilia mwenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 1.9.

Waliofikishwa katika mahakama hiyo ni pamoja na Nindwa Dindai na Mperwa Halili, ambao wote ni wakazi wa kijiji cha Matongo wilayani Busega.

Akiwasomea mashitaka yao mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Bunda, mheshimiwa Safina Simufukwe, mwanasheria wa Tanapa, Bw. Emmanuel Zumba, amesema kuwa washitakiwa hao wote kwa pamoja walikamatwa ndani ya hifadhi ya Serengeti machi 22, mwaka huu majira ya saa 4:00 asubuhi.

Bw. Zumba amesema kuwa washitakiwa hao walikuwa tayari wamekwishaua mnyama mmoja aina ya Pundamilia mwenye thamani ya shilingi 1,920,000, kwa kutumia pikipiki yenye namba za usajili T. 111 AMG pamoja na kisu pamoja na panga.

Amesema kuwa washitakiwa wote ni wawindaji haramu sugu ambao wamekuwa wakitumia pikipiki kufukuza wanyama na kwamba mnyama anapochoka na kusimama ndipo washitakiwa hao umshambulia kwa silaha mbalimbali za jaidi na kumuua.

Aidha, amesema kuwa washitakiwa hao wameshitakiwa kwa makosa manne, ikiwa ni pamoja na kuingia hifadhini kinyume cha sheria, kukamatwa na nyara ya serikali, kuingia na silaha hifadhini na kuua mnyama hifadhini bila kibali cha mamlaka husika.

Washitakiwa wote wamekana mashaitaka yao na wamenyimwa dhamana na kupelekwa mahabusu hadi Aprili 4 mwaka huu, kesi yao itakapotajwa tena mahakamani hapo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa