Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
ZAIDI ya wananchi 40,00 kutoka vijiji 12
wilayani Serengeti Mkoa wa Mara wanataraji kunufaika na mradi wa Maji
unaotekelezwa wilayani hapo kwa ufadhili wa Benki ya Dunia kwa zaidi y
ash.bilioni 4.
Mhandisi wa Maji wilaya hiyo Bw.Muraza Marwa amesema kuwa mradi huo ulioanza kutekelezwa mwaka 2010 utakamilika mwaka huu,na baadhi ya vijiji mradi umeishakamilika ikiwa ni awamu ya kwanza ya utekelezaji.
Muraza amesema katika awamu ya kwanza vijiji vya
Masangura,Parknyigoti,Motukeli,Mbalibali na Natta mbisso mradi umekamilika ,huku awamu ya pili ihusisha vijiji vya
Nyamitita/Kenyana,Rung'abure,Kebanchabancha,Nyagasense,Nyansurumunti na Wagete ,miradi hiyo iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
Katibu tawala wa Mkoa wa Mara Bwana Benedicti Ole Kuyan akizindua mradi wa maji katika kijiji cha Park nyigoti ,ikiwa ni wiki ya maji amewataka wananchi kuhakikisha wanatunza vyanzo vya maji,ili viweze kuwahudumia kwa muda mrefu.
Kilele cha siku ya wiku ya maji Kimkoa kitafanyikia kijiji cha
Mbalibali wilayani Serengeti.
0 comments:
Post a Comment