Home » » WANAFUNZI KORTIN KWA KUMJERUHI MWALIMU

WANAFUNZI KORTIN KWA KUMJERUHI MWALIMU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
WANAFUNZI wawili wa Shule ya Sekondari Kibara, iliyoko wilayani Bunda, Mara, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bunda wakikabiliwa na tuhuma za kumshambulia mwalimu mkuu wa shule hiyo na kumjeruhi kwa panga sehemu mbalimbali mwilini.
Waliofikishwa mahakamani jana ni Amos Shirima (22), mkazi wa Kijiji cha Kibara na James Athuman (22) mkazi wa Kijiji cha Namibu, wilayani Bunda.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Safina Simufukwe, Mwendesha Mashitaka, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Masoud Mohamed,  alidai kuwa washitakiwa walitenda kosa hilo Machi 17, saa 5 asubuhi, baada ya kumvamia mwalimu huyo ofisini kwake
 Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa