Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
JESHI la Polisi Rorya linamshikilia Mwenyekiti wa Kijiji cha
Marasibora, Kata ya Kisumwa, Sproza Charles, kwa tuhuma za wizi wa
ng’ombe watatu wa ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa
Arusha, Aden Kagose.
Mwenyekiti huyo alifikishwa katika kituo cha Polisi Komoswa jana
baada ya kudaiwa kushirikiana na wenzake watatu ambao ni Hamis
Nyamaganda, Mwita Mwita na Werema Nyamaganda wakazi wa Marasibora,
kuiba ng’ombe hao.
Watuhumiwa Nyamaganda na Werema wanaendelea kusakwa na polisi baada ya kutorokea kusikojulikana.
Kamanda wa Polisi Mkoa, Justus Kamugisha, aliwaambia waandshi wa
habari kwamba mwenyekiti wa kijiji hicho aliingia kwenye tuhuma hiyo
baada ya kuidhinisha barua ya kuhalalisha ng’ombe hao wa wizi kuuziwa
Mwita.
Alisema mwenyekiti huyo aliidhinisha barua ya kuuzwa ng’ombe hao
wenye thamani ya sh 1,800,000 kutoka kwa watuhumiwa Matiko Nyamaganda na
Werema Nyamaganda bila kuthibitisha uhalali wa umiliki wake.
Jeshi hilo lilifanikiwa kuwakamata mwenyekiti na Mwita muda mfupi na
kufikishwa kituo cha Polisi cha Komaswa ambapo watafikishwa mahakamani
kesho.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu, mmiliki wa ng’ombe
hao, Kagose, alikiri kuibwa ng’ombe hao na kwamba anasubiri taratibu za
kisheria kufuatwa ili watuhumiwa wafikishwe mahakamani.
Kagose anayewakilishwa na ndugu yake katika suala hilo, alisema alipewa taarifa ng’ombe wake wameibiwa na watu hao.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment