Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mchango wa
shilingi elfu moja Mzazi kwa ajili ya Ujenzi wa Choo katika Shule ya
Msingi Sirari Wilayani Tarime Mkoani Mara umekuwa kizaa zaa ktika
Mkutano wa Serikali ya Kijiji uliofanyika jana katika Shule hiyo.
Baadhi ya Wazazi
hao wameshindwa kulipa kiwango hicho kwa ajili ya kusukuma gurudumu
la Maendeleo katika Shule hiyo,suala ambalo lilipelekea jana kuongeza adhabu ya
kulipa shilingi elfu kumi kwa mtu ambaye alikuwa hajalipa shilingi elfu moja hapo
awali.
Shule ya Msingi
Sirari inakumbwa changamoto ya Upungufu wa vyoo suala amabalo ni
Changamoto kubwa kwa Wanafunzi hao.
Kupitia Mkutano
mkuu wa Serikali amabao ulifanyika uliadhimia kuchanga Shilingi elfu Moja kwa
ajili ya ujenzi wa Choo cha Shule ya Msingi suala ambalo limepelekea jana Wazazi ambao
hawajakamilisha Mchango wa kulipa faini ya Shilimngi Elfu kumi uku ikiundwa
kamati ya Wajumbe Sita ya kupitia Michango katika vijiji na vitongoji kwa lengo
la kubaini wananchi waliogomea Michango hiyo.
Hata hivyo wazazi
hao katika Mkutano huo wamemtaka Mwl mkuu wa Shule ya Msingi Sirari kuwasomea
Mapato na Matumizi kwani hapo awali Bodi ya Shule ilikuwa ikichangisha Michango
bila kushirikisha Serikali ya Kijiji na ndipo waliweza kusimamishwa zoezi hilo
la kuchangisha Michango hiyo baada ya Malalamiko kutoka kwa wazazi.
Kwa Upande wake
Mwenyekiti wa Kijiji Nyangoko Paul kupitia Mkutano huo amewataka
wenyeviti wote wa Vitongoji kutoa Ushirikiano wa kutosha kwa lengo la kubaini
wale wote waliogoma kuchanga Mchango huo.
Sanjari na hayo
Mwenyekiti huyo amewataka Wananchi hao kuondokana na kuchagua Viongozi kwa
ushabiki na hatimayake wanashindwa kutoa Ushirikiano katika Utendaji wa kazi.
Suala la
kushangaza na kuonesha kuwa jamii hjaitaki kujitolea mpaka kusukumwa baada ya
kikao hicho gradio Victoria hili lilifanikiwa kutembelea ofisi ya Ofisa
Mtendaji wa kata ya Sirari nakushudia Mamia ya watu wakiwea kwenye Mstali wa
kulipa shilingi elfu moja kwa kuogopa faini ya Shilingi Elfu kumi iliyoazimiwa
na Mkutano huo.
0 comments:
Post a Comment