Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SERIKALI
imeombwa kuzuia malipo ya posho kwa wabunge wa Bunge Maalumu la Katiba,
badala yake fedha hizo zielekezwe katika huduma za jamii.
Kauli hiyo ilitolewa juzi wilayani Rorya mkoani Mara na Makamu wa
Rais wa Vyama vya Walipa Kodi Duniani, Otieno Igogo, alipokutana na
wafanyakazi wa Shamba la Masista wa Baraki.
Igogo amesema hakuna sababu kwa serikali kutumia fedha za walipa kodi
kuwalipa wabunge hao ambao imedhihirika wazi kuwa hawawezi kuwapatia
Watanzania katiba bora waliyoitegemea.
“Tumeshuhudia kodi za Watanzania zikichezewa kwa kuendesha Bunge la
Katiba lililojaa vijembe, matusi, kejeli na ushabiki wa vyama.
“Hapa hakuna katiba mpya, badala yake ni vema serikali ikazitumika
kuokoa maisha ya wananchi kwa kununua dawa na vifaa tiba katika vituo
vya afya maeneo ya vijijini nchini,” alisema.
Shutuma za kiongozi huyo zimekuja kukiwa na shutuma kutoka kila kona ya nchi, juu ya mwenendo mzima wa Bunge hilo ulivyokwenda.
Akitoa taarifa za shamba hilo linaloendesha shughuli za kilimo na
ufugaji, mkuu wa shamba hilo, Sista Janepher Mabonyesho, amesema kuwa
pamoja na kituo hicho kutoa mchango mkubwa wa maendeleo, lakini
hakuna msaada wowote unatolewa na serikali kuunga mkono juhudi hizo.
Awali Paroko wa Parokia ya Baraki, Padri Alexander Choka, ameitaka
jamii kuacha kuilalamikia serikali kwa kila kitu bali watambua wajibu
wao wa kufanya kazi kwa bidii.
Akiwa katika shamba hilo, makamu huyo wa rais wa vyama vya walipa
kodi dunia, mbali na kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na
kituo hicho, imezindua tovuti na kutoa sh milioni 6 kwa ajili ya
kusaidia kituo hicho na chakula cha mwezi mzima kwa kituo cha watoto
wadogo katika kituo hicho.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment