Home » » SHULE YAFUNGWA BUNDA BAADA YA WATU KUJISAIDIA OVYO DARASANI

SHULE YAFUNGWA BUNDA BAADA YA WATU KUJISAIDIA OVYO DARASANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Shule ya Msingi Kibara B, iliyoko wilayani Bunda mkoani Mara, imefungwa na wananchi kwa muda kutokana na watu wasiofahamika kujisaidia kwenye vyumba vya madarasa, hali inayohatarisha afya za wanafunzi.
Mwenyikiti wa Kijiji cha Kibara B, Mafwili Mnyaga alisema kuwa shule hiyo imefungwa kwa muda usiojulikana tangu Aprili 28.
Alisema  shule hiyo, iliyoko katika Mji Mdogo wa Kibara, imefungwa na wananchi wa kijiji hicho baada ya walimu kukuta asubuhi kila chumba kimejaa vinyesi  milangoni, maeneo ya nje, pamoja na vyooni.
Aidha, alisema kuwa mbali na hali hiyo, pia mashimo ya vyoo hivyo yalikutwa yamezibwa kwa vitu vigumu, huku vinyesi vingine vikiwa kwenye ndoo za maji zinazotumiwa na wanafunzi kwa ajili ya kufanyia usafi.
Alisema kuwa, baada ya walimu wa shule hiyo ambayo iko katikati ya makazi ya watu, kukuta hali hiyo kwenye kila darasa walitoa taarifa  kwa uongozi wa kijiji hicho ambao ulichukua hatua ya kuifunga shule kwa muda.
“Baada ya kufika shuleni hapo na kufanya mkutano, wananchi  waliazimia kuwaruhusu watoto warudi nyumbani na kuifunga shule hiyo kwa muda,” alisema.
Aliongeza kuwa walichukua hatua hiyo kwa kuhofia watoto kuugua magonjwa yasiyofahamika kwani wanaofanya tukio hilo hulifanya usiku na pia hawajui madhumuni yao.
Tayari uongozi wa kijiji umeandika barua kwenda kwa mkurugenzi mtendaji wa wilaya na mkuu wa wilaya kuomba msaada na ufumbuzi wa suala hilo.
“Tumeifunga shule  kwa sababu hali hii ni mbaya na tatizo hili halikuanza leo na linafanyika nyakati za usiku.’’
Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa