WAFANYABIASHARA
wadogo hapa nchini wametakiwa kuchangamkia fursa za biashara
zinazotolewa na Kampuniya China World Buz iliyoanzishwa naWatanzania
waishio nchini China, itakayowawezesha kuagiza bidhaa mbalimbali kwa
mtaji kidogo walionao bila kuingia gharama ya kufuata bidhaa hizo nchini
China.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,
Bw.Justine Luvanda wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati
akitambulisha mradi huo katika mikoa mitatu hapa nchini.
Alisema
kuwa,lengola mpango huo ni kuwawezesha Watanzania wenye mtaji kidogo
kukuza mitaji yao kwa kuagiza bidhaa kutoka China bila kuingia gharama
ya kwenda kununua bidhaa hizo China kutokana na mitaji yao.
Bw.Luvanda
alisema kuwa iwapo elimu itawafikia wafanyabiashara hao itaweza
kuwanufaisha kwa kiasi kikubwa kwani baadhi yao wamekuwa na mitaji
midogo na kushindwa kujua wafanyebiashara gani kwa ajili ya kukuza
biashara zao.
Aliongeza kuwa,kupitia mpango huo wakibiashara
wafanyabiashara hao wataweza kuletewa bidhaa zao kutoka China na kwa bei
nafuu na kuuza nchini na kupata faida nzuri kwa kuongezea mitajiya o.
Alifafanua
kuwa, kupitia kampuni hiyo wataweza kupata elimu jinsi ya
kufanyabiashara zao na kuku zamitaji yao na kuwa na uhakika na usalama
wa bidhaa zao kwani pindi itakapotokea hasara yoyote katika uagizaji wa
biashara hizo zitalipwa na kampuni hiyo.
Naye afisa mtendaji mkuu wa
kampuni hiyo hapa Tanzania Bw.Shafii Swed alisema kuwa, kampuni hiyo ni
kampuni ya kwanza ya kitanzania kupata usajili wakibiashara
na ilifunguliwa rasmi na Rais wa China Xijin Ping kuwa eneo huru la soko la kimataifa la biashara.
Alisema
kuwa, kampuni hiyo ilifunguliwa ikiwa na lengo la kukuza na kuendeleza
mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na China ikiwa na lengo la
kutoa bidhaa China na kuziuza Tanzania huku wakichukua mali ghali na
kupeleka nchini China hali ambayo itasaidia kukuza soko la ajira hapa
nchini.
Akizungumzia changamoto wanayoipata wafanyabiashara
kuanzishwa kwa kampuni hiyo wamedai kuwa kutokana na kero wanazop ata
ikiwani pamoja na gharama za kufuatilia viza, usafiri, malazi na gharama
nyingine mbalimbali hivyo kupitia kampuni hiyo itawawezesha
kuwarahisishia kupata bidhaa zao kwa wakati
Chanzo:Majira
1 comments:
mawasiliano vp!?
Post a Comment