Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Tarime na Rorya, linamshikilia
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya
Rorya, Roger Kukuu kwa tuhuma za kujipatia sh milioni 11.5 kwa
udanganyifu.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Tarime na Rorya, Kamishina
Msaidizi Mwandamizi, Justus Kamugisha, alisema kiongozi huyo anadaywa
kujipatia fedha hizo kutoka kwa Paul Oyoo.
Alieleza kiongozi huyo alichukua fedha hizo kwa udanganyifu Januari 6
mwaka huu, baada ya kupata zabuni ya kutengeneza samani za Halmashauri
ya Rorya, lakini alishindwa kurejesha fedha hizo kama alivyotakiwa.
“Huyu mtu tunamshikilia kwa tuhuma za wizi wa kuaminika, kwani
alipopata tenda (zabuni) za kutengeneza fenicha za halmashauri ya Rorya
alichukua fedha kwa Paul Oyoi, lakini alipolipwa alishindwa kurejesha
fedha hizo,”alisema Kamanda Kamugisha.
Hata hivyo, alisema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi na
kwamba mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya, Samwel Kiboye, alipozungumza na
gazeti hili kwa njia ya simu alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo na
kusema chama hakihusiki kwa tukio hilo, hivyo kutaka vyombo vya dola
kuchukua hatua bila kujali cheo cha mtu ili haki iweze kutendeka.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment