Home » » WASSIRA ATANGAZA KUTETEA UBUNGE BUNDA

WASSIRA ATANGAZA KUTETEA UBUNGE BUNDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
“Ndugu wajumbe napenda kutumia nafasi hii kutangaza rasmi kwamba ninagombea tena ubunge wa jimbo hili. Wale wanaokereka wakereke tu. Nina nguvu bado za kuwatumikia Wanabunda.” Stephen Wassira  

Mbunge wa Jimbo la Bunda (CCM), Stephen Wassira ametangaza kuwa atatetea tena nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao, huku akijigamba kuwa yeye ni “mwarobaini wa matatizo” yanayowakabili wakazi wa jimbo hilo.
Kabla ya kutangaza nia hiyo jana, mara kadhaa Wassira amekuwa akihusishwa na suala la urais na ni mmoja wa makada sita wa CCM ambao walipewa adhabu na chama hicho, Februari 18, mwaka huu baada ya kukutwa na makosa ya kuanza mapema kampeni za urais mwaka 2015.
Wassira, ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) alitangaza uamuzi wake huo katika kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM wilayani Bunda kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo.
Wassira, ambaye ana umri wa miaka 69, aliwaponda wanaombeza kuwa amezeeka, hivyo kuweka wazi kwamba ameamua kuwania tena nafasi hiyo kwa sababu bado ana nguvu na uwezo wa kuwatumikia wananchi kwa kipindi kingine cha miaka mitano na kutimiza ndoto zao za kupata maisha bora kwa kila mmoja wao.
“Ndugu wajumbe napenda kutumia nafasi hii kutangaza rasmi kwamba ninagombea tena ubunge wa jimbo hili. Wale wanaokereka wakereke tu. Nina nguvu bado za kuwatumikia Wanabunda,”alisema Wassira.
“Nyote ni mashahidi kwa jinsi ninavyoshirikiana nanyi katika kuondoa changamoto zinazotukabili ambazo nyingi ziko karibu kuisha ili wote wapate maisha bora yaliyoahidiwa na CCM. Nawaombeni tu tuzidi kushirikiana,” alisema Wassira, ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM.
Pamoja na mwanasiasa huyo mkongwe, ambaye amekuwa waziri katika awamu tatu za urais, kujitahidi kwa kiasi kikubwa kuwaletea wakazi wa jimbo hilo, bado kuna changamoto katika sekta za afya, maji hasa kwa maeneo ya vijijini.
Wachunguzi wa mambo wanadai kuwa kama hatatimiza ahadi hiyo aliyoitoa wakati wa kampeni za mwaka 2005 na kuanza ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wa mji huo mwaka 2007, basi huenda akapata wakati mgumu kutetea nafasi hiyo.
Wassira anakuwa mwanachama wa kwanza wa CCM kutangaza wazi nia yake ya kuwania nafasi hiyo. Wengine wanaotajwatajwa kuuwinda ubunge huo ni mbunge wa viti maalumu (CCM), Ester Bulaya na mjumbe wa NEC wa wilaya hiyo, Bonifasi Mwita ambao bado hawajaweka wazi nia yao.
Wassira alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere na pia ameshawahi kuwa Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na baadaye kuwa Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo chini ya uongozi wa Ali Hassan Mwinyi.
Aliteuliwa kuwa Waziri wa Maji mwaka 2006 na baadaye kuhamishiwa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika na mwaka 2008 aliteuliwa kuwa Waziri wa Tamisemi. Mwaka 2010 Wassira aliteuliwa kushika wadhifa alionao sasa.Mbunge wa Jimbo la Bunda (CCM), Stephen Wassira ametangaza kuwa atatetea tena nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao, huku akijigamba kuwa yeye ni “mwarobaini wa matatizo” yanayowakabili wakazi wa jimbo hilo.
Kabla ya kutangaza nia hiyo jana, mara kadhaa Wassira amekuwa akihusishwa na suala la urais na ni mmoja wa makada sita wa CCM ambao walipewa adhabu na chama hicho, Februari 18, mwaka huu baada ya kukutwa na makosa ya kuanza mapema kampeni za urais mwaka 2015.
Wassira, ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) alitangaza uamuzi wake huo katika kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM wilayani Bunda kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo.
Wassira, ambaye ana umri wa miaka 69, aliwaponda wanaombeza kuwa amezeeka, hivyo kuweka wazi kwamba ameamua kuwania tena nafasi hiyo kwa sababu bado ana nguvu na uwezo wa kuwatumikia wananchi kwa kipindi kingine cha miaka mitano na kutimiza ndoto zao za kupata maisha bora kwa kila mmoja wao.
“Ndugu wajumbe napenda kutumia nafasi hii kutangaza rasmi kwamba ninagombea tena ubunge wa jimbo hili. Wale wanaokereka wakereke tu. Nina nguvu bado za kuwatumikia Wanabunda,”alisema Wassira.
“Nyote ni mashahidi kwa jinsi ninavyoshirikiana nanyi katika kuondoa changamoto zinazotukabili ambazo nyingi ziko karibu kuisha ili wote wapate maisha bora yaliyoahidiwa na CCM. Nawaombeni tu tuzidi kushirikiana,” alisema Wassira, ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM.
Pamoja na mwanasiasa huyo mkongwe, ambaye amekuwa waziri katika awamu tatu za urais, kujitahidi kwa kiasi kikubwa kuwaletea wakazi wa jimbo hilo, bado kuna changamoto katika sekta za afya, maji hasa kwa maeneo ya vijijini.
Wachunguzi wa mambo wanadai kuwa kama hatatimiza ahadi hiyo aliyoitoa wakati wa kampeni za mwaka 2005 na kuanza ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wa mji huo mwaka 2007, basi huenda akapata wakati mgumu kutetea nafasi hiyo.
Wassira anakuwa mwanachama wa kwanza wa CCM kutangaza wazi nia yake ya kuwania nafasi hiyo. Wengine wanaotajwatajwa kuuwinda ubunge huo ni mbunge wa viti maalumu (CCM), Ester Bulaya na mjumbe wa NEC wa wilaya hiyo, Bonifasi Mwita ambao bado hawajaweka wazi nia yao.
Wassira alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere na pia ameshawahi kuwa Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na baadaye kuwa Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo chini ya uongozi wa Ali Hassan Mwinyi.
Aliteuliwa kuwa Waziri wa Maji mwaka 2006 na baadaye kuhamishiwa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika na mwaka 2008 aliteuliwa kuwa Waziri wa Tamisemi. Mwaka 2010 Wassira aliteuliwa kushika wadhifa alionao sasa.
Chanzo:Mwananchi

0 comments:

Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa