Home » » MKANDARASI ATAKIWAKUMALIZA BARABARA KWA WAKATI

MKANDARASI ATAKIWAKUMALIZA BARABARA KWA WAKATI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, amemtaka mkandarasi Kampuni ya J.V anayejenga barabara ya Makutano-Nyamuswa-Ikoma Gate, sehemu ya Makutano-Natta kilomita 50, kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha mradi huo kwa wakati.
Waziri Magufuli alitoa tamko hilo jana wakati akihutubia mamia ya wakazi wa mjini Butiama, Mara.
“Najua bado mnaidai serikali zaidi ya shilingi bilioni tatu, lakini hii isiwe sababu ya kushindwa kuendelea na kazi japo mlishaonyesha mfano mzuri wa kuanza kujenga daraja la Kyarano,” alisema.
Pia aliahidi kuwa ndani ya wiki mbili atatafuta fedha kwa ajili ya kumlipa mkandarasi huyo, ili aweze kuendelea na kazi kwa kasi kubwa.
“Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara yupo hapa pamoja na wataalamu wangu, tutahakikisha ndani ya wiki mbili tutatafuta fedha kwa ajili ya kumlipa mkandarasi pamoja na fidia na kuondoa nguzo za umeme,” alisema Waziri Magufuli.
Pamoja na hayo, aliwatoa hofu wananchi wa Butiama kwa kusema kuwa wale wote waliofuatwa na barabara katika maeneo yao watafidiwa kama sheria inavyoeleza.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa