Home » » KIONGOZI WA NCCR AUWA SERENGETI

KIONGOZI WA NCCR AUWA SERENGETI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Kamishna wa NCCR-Mageuzi Mkoa wa Mara, Stephen Sebeki ameuawa kwa kukatwakatwa mapanga na mtu anayedaiwa kuwa ni hawara wa shemeji yake, chanzo kikidaiwa kuwa ni mgogoro wa nyasi za kuezekea.
Mkuu wa polisi wa Wilaya ya Serengeti, Pius Mboko alisema tukio hilo lilitokea jana saa 2:00 asubuhi katika Kijiji cha Rung’abure wilayani hapa.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho, Charles Kibure alisema Sebeki aliuawa kwa kukatwa na panga sehemu ya shavu la kushoto, kichwani kwa nyuma na kiganja cha mkono wa kushoto na kufariki dunia papo hapo.
Mmoja wa ndugu wa marehemu alisema Sebeki aliuawa baada ya shemeji yake (mke wa marehemu kaka yake) kuuza nyasi za Sebeki alizokuwa amezipanda kwa kazi mbalimbali.
Inadaiwa kuwa Sebeki alipomhoji shemeji yake huyo sababu za kuuza nyasi zake, alitukanwa.
“Kumbe ndani kulikuwa na hawara yake amelala akatoka na panga na kuanza kumshambulia,” alisema Kibure.
Alisema baada ya tukio hilo mtuhumiwa na hawara yake walikimbia, huku wakiwaacha watoto watatu na haijajulikana walipo.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Jacob Sendi alisema mtuhumiwa kwa muda mrefu amekuwa akiishi na shemeji yake.
Alisema polisi walimchukua shemeji mkubwa wa Sebeki, Mrembo Ngige ambaye alikuwapo wakati tukio hilo pamoja na watoto hao watatu ili kusaidia upelelezi
Chanzo:Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa