Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Timu ya riadha ya mkoa wa Mara huenda ikajitoa kushiriki kwenye
mashindano ya taifa ya riadha yatakayofanyika Jumamosi na Jumapili
jijini Dar es Salaam kutokana na kukosa Sh4 milioni za kufanikisha
ushiriki wao.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Mkoa
wa Mara, Dotto Bwire, kikosi hicho kilikuwa kiondoke jana mjini Musoma
kwa basi kuja Dar es Salaam, lakini kimekwama kusafiri kutokana na
kukosa nauli.
Bwire alisema wamehangaika kuomba misaada kwa
wadau mbalimbali wa mkoa huo ikiwamo wabunge na wakurugenzi wa
halmashauri zote nane za Mkoa wa Mara, lakini imeshindikana.
“Hadi sasa (jana jioni) hatuna hata senti tano,
hatujui timu yetu itafikaje Dar es Salaam kwenye hayo mashindano, kama
tutakwama basi hatuna budi kujitoa ingawa tutawanyong’onyeza wanariadha
wetu ambao kwa kweli wamejiandaa,” alisema Bwire.
Mwenyekiti wa chama hicho, Daniel Thomas, ambaye
pia ni miongoni mwa Watanganyika wa kwanza kushiriki Olimpiki, alisema
kikosi hicho cha mkoa kilichochaguliwa kwenye mashindano ya mkoa
yaliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Bunda kinaendelea na
mazoezi.
Thomas alisema timu hiyo ni ya mbio ndefu za mita 10,000 na 5,000, mbio za kati mbio fupi, relay, miruko na mitupo.
Chanzo:Mwnanchi
Chanzo:Mwnanchi
0 comments:
Post a Comment