Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MTOTO Lusia Moga (2) aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha
Julai 8, mwaka huu kati Kijiji cha Bukore wilayani Bunda, Mara amekutwa
akiwa mtupu nyumbani kwa Magembe Nyabu, mkazi wa kijiji hicho.
Kupatikana kwa mtoto huyo juzi alfajiri kuliibua hofu ya kuwepo kwa
ushirikina iliyotawala kwa wazazi wa mtoto huyo na wakazi wengine
kijijini hapo.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Bukore, Moshi Madeni, alisema licha ya
mtoto huyo kukutwa utupu, alikuwa amenyong’onyea kwa sababu ya njaa.
“Tulipomwona watu walijaa kumshuhudia, lakini mama yake alikataa
kumbeba hivyo mtoto huyo alibebwa na mtu mwingine. Kitu cha kwanza
alipewa uji kwa sababu alikuwa na njaa.
“Mpaka sasa mtoto huyo anaendelea vizuri, taarifa polisi tumepeleka
na hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusu tukio hilo,” alisema ofisa
mtendaji.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment