Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, amekiri mbele ya
viongozi wa serikali za vijiji saba vinavyozunguka mgodi wa dhahabu wa
North Mara, kuwa serikali ilifanya makosa na inastahili kulaumiwa
kutokana na adha wanazopata wananchi toka mgodini.
Chikawe alifikia hatua hiyo jana baada ya kupokea taarifa ya
malalamiko kutoka kwa viongozi wa serikali za vijiji na kata vya
Nyamwaga, Genkuru, Kewanja, Nyakunguru, Kerende, Matongo na Nyangoto,
ya kupigwa, kunyanyaswa, kuuawa, kujeruhiwa na kubambikwa kesi na
polisi.
Pia waziri huyo alielezwa jinsi mgodi wa Kampuni ya Afrika Barrick ya
Canada, ulivyoshindwa kuwafidia wananchi ili wahame na wale wote
waliofanyiwa uthamini na kikosi kazi mwaka jana, katika vijiji vya
Kewanja, Nyakunguru na Nyangoto, kuendelea kuwepo wakipata adha.
Malalamiko hayo kwa Chikawe aliyeambatana na Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini (IGP), Ernest Mangu, yalitolewa Diwani wa Kata ya Kemambo,
Willison Mangure na mwenzake wa viti maalum Matongo Tontora
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment