Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SHULE ya sekondari Hunyari iliyoko katika Wilaya ya Bunda mkoani
Mara, inakabiliwa na changamoto ya utoro mkubwa wa wanafunzi kutokana na
baadhi yao kukatisha masomo kwa kuo, kuolewa na wengine kuchunga
mifugo.
Taarifa hiyo ilitolewa jana na mkuu wa shule hiyo, Joachim Kishai,
mbele ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Wilaya ya Bunda,
Boniphace Mwita aliyetembelea shule hiyo.
Kishai alisema kuwa shule hiyo yenye kidato cha kwanza hadi cha nne,
inakabiliwa na changamoto hiyo ya utoro wa wanafunzi unaosababishwa na
baadhi yao kubeba mimba, kuoa, kuolewa na kufanya shughuli za uchungaji
wa mifugo.
Alifafanua kuwa kwa mfano, wanafunzi wa kidato cha nne walianza
kidato cha kwanza wakiwa 188, lakini hadi sasa wamebakia wanafunzi 44
tu.
Alisema kuwa kwa upande wa kidato cha tatu walioanza ni 280, lakini
waliopo kwa sasa ni 104 na kidato cha pili walioanza ni 136 waliopo ni
121.
Aliongeza kuwa kuwa hali hiyo husababishwa na wazazi kutotilia
umuhimu elimu kwa watoto wao, kwani baadhi yao uozwa ama kuoa, bila
wazazi kuchukua hatua yoyote ile na kuona jambo hilo kama la kawaida tu.
Alisema kutokana na hali hiyo, uongozi wa shule hiyo umekuwa
ukichukuwa hatua, ikiwa ni pamoja na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola
ama mahakamani wazazi wa aina hiyo.
Naye Mwita, alisema kuwa watashirikiana na halmasahuri ya wilaya hiyo
kupitia idara ya elimu kuanzisha opelesheni ya kuwasaka watoro.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment