Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Tarime/Rorya mkoani Mara, Lazaro Mambosasa
Kamanda Mambosasa amesema atafanya hivyo kwa kushirikisha mabaraza ya jadi (Ritongo) ,ulinzi shirikishi na raia wema wanaochukia uhalifu kwa kuwa watawawafichua wahalifu hata wale wanaotoka nchi jirani kwa kushirikiana na Watanzania.
Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na NIPASHE mwishoni mwa wiki.
Kamanda Mambosasa alisema: "Tumeanza kufanya mikutano ya hadhara katika kila kijiji katika wilaya zetu hizi mbili za Tarime na Rorya na mada kuu zikiwa ni kuimarisha ulinzi kwa kuwashirikisha wazee wa mila, walinzi shirikishi sungusungu , raia wema kwa kushirikiana na askari polisi jamii katika kila kata kufanya utafiti na kuwafichua wahalifu wanaotumia silaha za aina mbalimbali."
Aliongeza: "Kipindi kifupi cha kuishia mwezi uliopita katika msako wa siku tatu kuanzia Julai 25, mwaka huu, tuliteketeza ekari 16 za bangi katika vijiji vya Kubiterere na Remagwe."
Hata hivyo, Kamanda Mambosasa alisema walimaji na wamiliki wa mashamba hayo kutoka Nyankongo Sererya na Ngwena Masiaga, walitoroka kabla ya kukamatwa na polisi wanaendelea kuwasaka.
Kwa mujibu wa Kamanda Mambosasa, soko kubwa la zao hilo liko nchi jirani ya Kenya ambapo inadaiwa kuwa baadhi ya wafanyabiashara hutoa fedha kwa ajili ya kilimo cha bangi nchini Tanzania.
"Huwatumia mawakala wao na inapokomaa huvuna na kuisafirisha nchini Kenya na nyingine kwenda mikoa ya Kanda ya Ziwa hususani jijini Mwanza," alisema.
Alisema kuwa taarifa za kilimo cha zao hilo zinaonyesha kwamba wakulima wengi wapo katika vijiji vya Nkongore, Nyasaricho, Remagwe, Kubiterere, Kekomori, Ikoma, Kogaja, Tagota, Nyarwana, Nkende, Turwa, Nyandoto, Bumera, Kitenga, Kitagasembe, Pembe, Kemange, Gamasara, Mriba, Kimusi, Nyamwaga, Korotambe, Kiongera, Nyamohonda na Buhemba.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment