Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkazi
wa kijiji cha Kewanja Nyamongo, tarafa ya Ingwe, wilayani hapa, James
Ingramu (26), amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela, baada ya kukiri
mahakamani kumuua kwa panga shemeji yake, Makorere Makima.
Ingramu alimuua shemeji yake baada ya kuingilia ugomvi kati ya marehemu huyo na mke wake ambaye ni dada yake, Ghati Makorere.
Akisoma hukumu hiyo juzi katika Mahakama Kuu kilichofanyika Mahakama ya Wilaya Tarime, Mkoani Mara, Jaji wa Mahakama Kuu ya Mwanza, Aishi Sumari, alisema Ingramu baada ya kukiri kumuua shemeji yake kwa panga akimtetea dada yake, Mahakama inamtia hatiani na kumhukumu kutumikia kifungo cha miaka 10 jela kwa kuua bila kukusudia.
“Baada ya kukiri kosa na mahakama kukuona una hatia ya kuua bila kukusudia, nakuhukumu kwenda jela miaka 10 ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia mbaya kama yako,” alisema Jaji Sumari.
Awali wakili wa Serikali, Kainunuru Anisius, alidai mtuhumiwa James Ingramu alitenda kosa hilo la mauaji Oktoba 6 mwaka jana katika kijiji cha Kewanja Nyamongo wakati marehemu akigombana na mke wake Ghati, hali iliyomfanya mtuhumiwa achukue panga na kumkata kichwani Makorere kwa lengo la kumtetea dada yake.

CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment