Home » » SALAM ZA RAMBI RAMBI KUTOKA TONE MULTIMEDIA GROUP KUTOKANA NA AJALI ILIYOTOKEA MUSOMA LEO.

SALAM ZA RAMBI RAMBI KUTOKA TONE MULTIMEDIA GROUP KUTOKANA NA AJALI ILIYOTOKEA MUSOMA LEO.



Picha kwa Hisani ya Father Kidevu Blog

Tone Multimedia Group ambao ni wamiliki wa Mtandao wa Blogs zamikoa Tanzania, Tone Radio-Tz, This Day Magazine na Matukio na wanavyuo, Tumepokea kwa masikitiko makubwa Taarifa za Ajali mbaya iliyotokea Musoma Ambayo ilihusisha  Basi la J4 Express  T677CYC lililokuwa linatoka Sirari kwenda Mwanza limegongana uso kwa uso na basi la Mwanza Coach T736AWJ  Tarehe 5.09.2014 Majila ya Mchana katika eneo la sabasaba Musoma wakati moja ya mabasi hayo likiovateki basi lengine  ambapo  watu zaidi ya 39 wamepoteza maisha huku wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa. Mpaka sasa Maiti 25 zimetambuliwa kati ya 39 na ndugu wa Marehemu.

Tunaungana na watanzania wote kuwapa pole ndugu waliopotelewa na Ndugu, Jamaa na Marafiki waliopoteza ndugu zao katika ajali hii, Pia tunawapa pole wale Majeruhi wote Tunawaombea kwa Mungu wapate kupona Haraka ili tuje kuweza kuungana nao katika Kujenga Taifa.

Imetolewa na uongozi
Tone Multimedia Group





Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa