Home » » MTOTO APOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA

MTOTO APOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MTOTO Baraka John (13) mwanafunzi wa shule ya msingi Hunyari katika Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, amepotea katika mazingira ya kutatanisha, wakati akiwa nyumbani kwao.
Mzazi wa mtoto huyo ambaye pia ni Mganga katika Zahanati ya kijiji hicho John Tuoro, alisema mtoto huyo alipotea tangu Agosti 18 mwaka huu majira ya saa moja asubuhi.
 Alisema Baraka mara kwa mara alikuwa hataki shule na licha ya kumlazimisha kila mara lakini hakuacha utoro
Alisema katika kipindi cha mwezi mmoja alichokwenda shule Baraka alikuwa ameandika kwenye karatasi moja tu kwenye daftali moja.
Aliongeza kuwa siku ya kupotea kwake mtoto huyo aliondoka nyumbani hapo na kutokomea kusikojulikana akiwa amebeba baadhi ya nguo zake na kwamba siku hiyo alikuwa amevaa nguo aina ya tisheti nyekundu, suruali ya kaki na viatu aina ya eboebo vyenye rangi ya kilimu.
 Alisema kuwa mwanaye huyo umbo lake ni mwebamba mwenye urefu wa futi  3 na nusu, na ni mwenye rangi  ya maji ya kunde na kwamba anajua kuongea lugha mbili za Kiswahili na kijaruo .
Aliongeza kuwa alimtoa kwa mama yake mzazi huko Morogoro akiwa na umri wa miaka saba na kwamba hapo nyumbani kwake alikuwa akilelelewa na mke wake mwingine.
Alisema kuwa tukio la kupotea kwa mtoto huyo limeripotiwa polisi katika kituo cha Mugeta Wilayani hapa na ameomba mtu yeyote atakayemuona wawasiliane naye kwa namba yake ya simu 0765863660, ama ya bibi yake 0786583288 au ya babu yake 078479+5847.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa