Jeshi
la polisi mkoa wa Mara kwa kushirikiana na wenzao wa nchi jirani ya
Kenya wamefanikiwa kuwakamata watu wawili kwa tuhuma za kumwiba mtoto
Diana Meshack mwenye umri wa miezi saba mkazi wa makoko katika
manispaa ya musoma kisha kuficha katika nchi hiyo jirani huku waibaji
hao wa mtoto wakiomba kupewa fedha kiasi cha shilingi milioni tatu ili
waweze kumrejesha motto huyo.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mara kamishna msaidizi wa jeshi la
polisi ACP Philip Alex Kalangi, amesema kuwa mfanyakazi wa ndani
Paulina Sobe alikula njama na kutoweka na mtoto huyo hadi nchini Kenya
kabla baadhi ya watuhimiwa hao kuanza kumpigia simu mama mzazi wa
mtoto Bi Gaudioza Meshack wakitaka kutoa kiasi cha shilingi milioni
tatu ili waweze kumrejesha mtoto huyo.
Kamanda Kalangi amewataja watuhumiwa ambao tayari wamekamatwa
wakiwa na mtoto huyo huku akisema mfanya kazi wa ndani bado anatafutwa
na kwamba taratibu zimefanyika za kuleta watuhumiwa nchini kwa ajili
ya hatua zaidi za kisheria.
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la matukio ya
wizi wa watoto ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watu wakiwemo
wafanyakazi wa ndani na baada kufanya vitendo hivyo wameku wa
wakilazimisha kupewa fedha kama moja sharti la kurejesha watoto katika
familia zao.
Chanzo:ITV Tanzania
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment