Home » » TONE NA KILIMO:FAHAMU JUU YA USTAWISHAJI WA ZAO LA KABICHI NA FAIDA ZAKE KATIKA KUKUPATIA KIPATO , SOMA HAPA

TONE NA KILIMO:FAHAMU JUU YA USTAWISHAJI WA ZAO LA KABICHI NA FAIDA ZAKE KATIKA KUKUPATIA KIPATO , SOMA HAPA





UTANGULIZI:

Zao la kabichi hulimwa katika mikoa ya Morogoro, Arusha,Tanga, Iringa, Kilimanjaro na Mbeya.Kama mboga zao la kabichi lina viini lishe kama chokaa, protini, kambakamba na maji kwa wingi. Hutumika kutengeneza kachumbari, pia kuchanganywa na nyama au maharage.


II.HALI YA HEWA

Zao la kabichi hupendelea:-
- hali ya ubaridi Mwinuko: Kuanzia mita 1200 hadi 1900 kutoka usawa wa bahari.

Udongo: -
- Tifutifu
 - Rutuba nyingi
 - Unaohifadhi unyevu kwa muda mrefu
- Usiotuamisha maji
- Usio na chumvichumvi nyingi.
- Kama hauna rutuba ya kutosha ongeza mbolea ya samadi au mbolea vunde.


III. AINA ZA KABICHI· 

Early Jersey Wakefield: 

- Umbo lilochongoka kidogo,
- Hufunga vizuri,
- Uzito ni kati ya kilo 1.5 hadi 2.0,
- Hukomaa mapema siku 90 – 100 tangu kupandikiza.

· Copenhagen Market:

- Vichwa vya mviringo na hupasuka kirahisi
- Hukomaa mapema, siku 90 – 100 tangu kupandikiza· 

Prize Drumhead: 

- Vichwa vikubwa (kilo 2- 2.5),
- Vichwa ni bapa, huchelewa kukomaa (siku 110 – 120)
- Huvumulia hali ya jua kali
- Pia vichwa hupasuka.

· Oxheart: 

- Vichwa vidogo huchongoka kama moyo,
- Hupendwa sana na walaji,
- Ladha yake ni tamu, hukomaa mapema,
- Hazina tabia ya kupasuka.

· Glory of Enkhuizen: 

- Vichwa vya mviringo,
- Huvumilia hali ya jua kali,
- Huchelewa kukomaa (siku 110– 120)
- Ina tabia ya kupasuka.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa