Home » » MAMA MARIA NYERERE ASEMA BADO YUKO FITI NA AKANUSHA UVUMI ULIOENEA JANA KUWA AMEFARIKI DUNIA

MAMA MARIA NYERERE ASEMA BADO YUKO FITI NA AKANUSHA UVUMI ULIOENEA JANA KUWA AMEFARIKI DUNIA

Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere leo amezungumza na waandishi wa habari,nyumbani kwake Msasani jijini dar es salaam juu ya uvumi ulioenea nchini kuwa amefariki Dunia.

Mama Maria amewathibitishia watanzania kuwa bado yu hai na mwenye nguvu hivyo wasiwe na hofu nae. Alisema jana amepokea simu nyingi sana kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo watoto zake, wake wa watoto zake wote, familia yake pamoja na watu mbalimbali ili kumjulia hali.

Amesema alipopokea taarifa hizo wala hakushtushwa badala yake alifanya sara kwani uvumi huo wawezekana inatokana na vuguvugu la uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, pia utandawazi uliopo wa sayansi na teknolojia wa karne ya 21.

"jana nilipokea simu nyingi sana kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo watoto wangu, wake wa watoto zangu, pamoja na familia,walikuwa wakinisalimia, wengine waliposikia sauti yangu walikata simu" alisema Mama Maria.

Mama Maria alisema taarifa hizi za kuzushiwa kifo si mara ya kwanza kwani hata miaka ya nyuma akiwa na hayati baba wa Taifa, mwalimu Julius Nyerere walipokea taarifa nyingi za uvumi wa kifo.


Mjane wa hayati Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) nyumbani kwake Msasani jijini dar es salaam leo,juu ya uvumi wa kufariki Dunia ulioenea jana kupitia simu na mitandao ya kijamii.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa