Mahakama
kuu kanda ya Mwanza Januari 25 mwaka huu inatarajia kutoa uamuzi mdogo
wa kesi ya uchaguzi mkuu iliyofunguliwa na wakazi watatu wa jimbo la
Bunda mjini dhidi ya mbunge wa jimbo hilo Mh. Esther Bulaya, baada ya
hoja za kisheria za mawakili wa pande zote mbili kumalizika.
Kesi
hiyo ya uchaguzi namba 1 ya mwaka 2015, inasikilizwa na jaji wa
mahakama kuu kanda ya Mwanza Mh. Gwae, huku mjibu maombi wa kwanza Mh.
Esther Bulaya akitetewa na wakili Tundu Lissu, wakati msimamizi wa
uchaguzi wa jimbo la Bunda ambaye ni mjibu maombi wa pili na mwanasheria
mkuu wa serikali mjibu maombi wa tatu akitetewa na wakili Paschal
Malongo.
Walalamikaji
katika kesi hiyo ambao ni magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes
Ezekiel na Ascetic Malagila wanatetewa na mawakili wawili ambao ni
Costantine Mtalemwa na Denis Kahangwa.
Walalamikaji
hao wanadai kuwa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana
haukuzingatia sheria na taratibu kwani mgombea wa chama cha mapinduzi
Stephen Masato Wassira aliomba kura zihesabiwe upya akakataliwa na pia
hakupewa nakala ya matokeo.
Ikumbukwe kuwa Jaji Mkuu alitoa siku 90 kwa kesi zote zinazohusu
uchaguzi mkuu wa Octoba 25 kukamilika ili viongozi wakaendelee na
majukumu ya kutatua kero za wananchi.
0 comments:
Post a Comment