Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MWANAMKE mmoja aliyefahamika kwa jila la Elizabeth Mugendi (24),
mkazi wa Kijiji cha Kamugesi, Tarafa ya Makongoro, Wilaya ya Butiama
mkoani Mara, amewaua watoto wake wawili kwa kuwanywesha sumu kutokana na
ugomvi na ndugu yake.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Musoma jana, Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mara, Philip Kalangi, alisema tukio hilo lilitokea
Januari 16, mwaka huu katika kijiji hicho ambapo watoto hao walifariki
dunia walipofikishwa hospitali.
Alisema mama huyo baada ya kuwanywesha sumu watoto wake hao, Nicolaus Mauma (4) na Wanzagi Katoki (2) naye alikunywa sumu kwa lengo la kujiua.
Alisema mama huyo baada ya kuwanywesha sumu watoto wake hao, Nicolaus Mauma (4) na Wanzagi Katoki (2) naye alikunywa sumu kwa lengo la kujiua.
Kamanda Kalangi alisema kutokana na maelezo ya mwanamke huyo ambaye
anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Butiama baada
ya kuwanywesha sumu watoto wake, alichukua uamuzi huo kutokana na
kunyanyaswa na ndugu yake.
Alisema mwanamke huyo kutokana na maelezo yake, alidai ndugu yake
aliyemtaja kwa jina la Warioba Mugendi, amekuwa na tabia za kumpiga kila
wakati na uamuzi aliochukua alitaka kuondoka duniani yeye na watoto
wake ili ajiepushe na manyanyaso.
Kamanda Kalangi alisema kabla ya tukio hilo, ndugu yake huyo alimpiga sehemu mbalimbali za mwili wake kutokana na kuangusha glasi.
“Mwanamke huyu amewanywesha sumu watoto wake inayodaiwa ni ya kuulia wadudu na yeye mwenyewe kunywa kutokana na kile alichodai ugomvi aliokuwa nao yeye na ndugu yake.
“Tulipata taarifa hizi na kuzifuatilia ambapo baada ya kufikishwa hospitalini watoto walifariki dunia wakiwa wanapatiwa matibabu na mama yao bado anaendelea kupata matibabu akiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi,” alisema Kalangi.

CHANZO MTANZANIA.
0 comments:
Post a Comment