Home » » WAHIMIZWA KUANZA KUFUGA SAMAKI KWENYE VIZIMBA.

WAHIMIZWA KUANZA KUFUGA SAMAKI KWENYE VIZIMBA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


WANANCHI wametakiwa kuanza kutumia fursa ya kufuga samaki katika mabwawa na vizimba ziwani ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa samaki katika Ziwa Victoria unaotokana na uvuvi haramu.
Uvuvi huo haramu ni wa kutumia sumu na zana zisizoruhusiwa katika uvuvi. Ushauri huo ulitolewa juzi na 

Mkurugenzi Msaidizi wa Miradi ya UNDP Tanzania, Amon Manyama, wakati akikagua miradi ya ufugaji wa samaki inayofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi cha 822 KJ Rwamkoa, katika Mkoa wa Mara, kwa ufadhili wa shirika hilo la kimataifa.

Alisema kuwa teknolojia hiyo ya ufugaji wa samaki itawasaidia wananchi kujipatia kipato na kujiinua kiuchumi, huku akisisitiza wananchi kuachana na uvuvi haramu, kwani umesababisha samaki kupungua katika ziwa hilo kwa kasi kubwa.

Manyama alisema kuwa UNDP imeamua kufadhili kikosi hicho na kuanzisha miradi hiyo ya ufugaji wa samaki kwenye mabwawa, pamoja na kwenye vizimba ziwani, teknolojia inayofanyika katika nchi nyingi duniani.

Alisema kutokana na upungufu huo wa samaki ziwani humo, ni vema sasa wananchi wakaachana na uvuvi waliouzoea na badala yake wakajikita katika ufugaji wa samaki, ili wajiongezee kipato na kupata lishe bora.

Alisema kuwa UNDP wamekuwa wakitoa misaada mbalimbali hapa nchini na kwa mataifa mengine na kwamba tangu ianzishwe sasa imetimiza miaka 50.

Akitoa taarifa ya miradi ya ufugaji wa samaki katika kikosi hicho, Mkuu wa Kikosi, Mkinga Kinana, alisema kuwa awali walikuwa wakiendesha shughuli za uvuvi wa kawaida, lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na uvuvi haramu, samaki katika ziwa hilo wamepungua sana hali iliyosababisha wabadilike na kuanza ufugaji wa samaki kutokana na ufadhili wa UNDP.

Aliishukuru UNDP kwa ufadhili huo na pia akatumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kufika kwenye kikosi chao kupata elimu hiyo ya ufugaji samaki, ili wajiongezee kipato na kuondokana na umaskini.

Mtaalamu wa uvuvi katika kikosi cha 822 KJ Rwamkoma, Maulid Maulid, pamoja nam Kaimu Kamanda wa kikosi hicho, Peter Kulyakwaze, walisema kwa nyakati tofauti kuwa wanafuga samaki aina ya sato na kambale kwenye mabwawa yaliyoko kwenye kambi yao iliyoko katika kijiji cha Bulamba.
Walisema pia kuwa wanafuga sato kwenye vizimba vilivyoko ndani ya Ziwa Victoria katika mwalo wa kijiji cha Karukekere wilayani Bunda. Aidha sato na kambale wanaofugwa kambini walisema wanavunwa Juni mwaka huu.
CHANZO: GAZETI LA HABARI LEO.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa