Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na
mkandarasi Nyanza Road Works anayejenga barabara ya Bulyamba-Kisolya
yenye urefu wa Km 51. (Wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda Bw.
Joshua Mirumbe.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akizungumza na
wananchi wa kijiji cha Kisolya kuhusu ujenzi wa mradi wa barabara ya
Bulyamba-Kisolya yenye urefu wa Km 51 inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Muonekano
wa barabara ya Bulyamba-Kisolya yenye urefu wa Km 51 inayojengwa kwa
kiwango cha lami ambayo ni sehemu ya barabara ya Nyamuswa-Bunda hadi
Nansio Km 121.9.
Meneja
wa uwanja wa ndege wa Musoma Bi. Bertha Bankwa akifafanua jambo kwa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa katika
mkutano wa watumishi wa sekta zilizo chini ya Wizara hiyo.
Daraja
la reli linaloingia baharini katika bandari ya Musoma kupokea na
kupakia mizigo kwenye melikwa ajili ya kuisafirisha katika maeneo
mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewataka
watendaji walio chini ya Wizara yake kuongeza kasi ya kukusanya mapato
ili kuwezesha malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kukuza uchumi na
kuboresha maisha ya wananchi kufikiwa kwa wakati.
Akizungumza
na watumishi wa sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilino mjini Musoma,
Prof. Makame Mbarawa amesema kufanya kazi kwa umoja, uadilifu, uwazi na
ubunifu kutasababisha kufikiwa kwa malengo hayo mapema.
“Kama
mtu hawezi kufanya kazi kwa kasi na kwa malengo yanayotekelezeka na
kupimika atupishe kabla hatujamuondoa, hatuta muonea mtu na
hatutamvumilia mtu atakayeshindwa kuendana na kasi yetu”, amesema Waziri
Prof. Mbarawa.
Prof.
Mbarawa amesema Serikali imetenga zaidi ya dola milioni 30 kwa ajili ya
kukarabati uwanja wa ndege wa Musoma na kununua magari ya kisasa ya
zimamoto ili kurudisha hadhi ya uwanja huo.
Aidha,
amezitaka taasisi za Serikali zinazodaiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme
(TEMESA), mkoani Mara kulipa madeni yao ili kuuwezesha wakala huo
kufanya kazi kwa kasi na kufikia malengo yaliyowekwa.
Katika
hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa barabara ya
Makutano-Nata-Mto wa Mbu yenye urefu wa km 467.7 inayojengwa na
makandarasi wazalendo kumi na kutaka mkandarasi anayejenga kipande cha
km50 kutoka Makutano hadi Sanzate kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa
haraka ikiwemo daraja la kyarano ili kuiwezesha barabara hiyo kupitika
wakati wote wa mwaka.
Amemwagiza
Meneja Wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa Mara Eng. Emmanuel Koroso
kuhakikisha makandarasi wanaojenga barabara mkoani humo wanarejea
kazini kwa kuwa serikali imeanza kulipa madai yao.
Ameitaka
Halmashauri ya Wilaya ya Butiama kutumia fedha zilizotumwa kutoka Mfuko
wa Barabara (RFB) kutumika kwa miradi iliyokusudiwa ili kuingunisha
wilaya hiyo mpya na wilaya nyingine mkoani Mara kwa barabara za lami.
Akiwa
wilayani Bunda Prof. Mbarawa amemtaka mkandarasi Nyanza Road Works
anayejenga barabara ya Buliamba-Kisolya Km 51 kuendelea na ujenzi wa
barabara hiyo kwa mujibu wa mkataba kwani serikali imeshalipa fedha
shilingi bilioni 8.5 kwa ajili ya barabara hiyo ambayo ni sehemu ya
barabara ya Nyamuswa-Bunda-Kisolya-Nansio yenye urefu wa Km 121.9.
Aidha,
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Mbarawa amewataka
viongozi wa Wilaya za Magu, Bunda na Musoma kufanya kampeni kubwa ya
kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kulinda Miundombinu ya Barabara, Reli
na Mkongo wa taifa wa Mawasiliano ili isihujumiwe na kusababisha
usumbufu kwa jamii na kuisababishia serikali hasara.
Naye,
Mbunge wa Mwibara Mhe. Kangi Lugola amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa
kuwa kukamilika kwa barabara ya Nyamuswa-Bunda-Kisolya hadi Nansio
yenye urefu wa KM 121.9 itasaidia kukuza uchumi wa Wilaya ya Bunda na
Ukerewe kwa kuwa eneo hilo lina shughuli nyingi za uchumi zinazotokana
na kilimo, ufugaji na uvuvi wa Samaki.
Prof.
Mbarawa amewataka makandarasi wote nchini kuhakikisha wanawapa
wafanyakazi wao mikataba kulingana na sheria za nchi ili kuwezesha
miradi ya barabara inayoendelea kujengwa kukamilika kwa wakati na
kuondokana na hujuma zinazoweza kudhoofisha ujenzi wa barabara na
miundombinu mingine.
“Lindeni
miundombinu ili idumu kwa muda mrefu, barabara, reli na mkongo wa taifa
ni miongoni mwa miundombinu inayojengwa kwa fedha nyingi na kuhujumiwa
mara kwa mara hivyo kuisababishia Serikali hasara”, amesisitiza Prof.
Mbarawa.
Waziri
Prof. Mbarawa yupo kwenye ziara ya kukagua Ujenzi wa miundombinu ya
barabara, bandari na mkongo wa taifa wa mawasiliano katika mikoa ya
kanda ya ziwa ambapo ametembelea Wilaya za Magu, Bunda, Butiama na
Musoma
0 comments:
Post a Comment