Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara, Bibi. Janeth
Mayanja amemsimamisha kazi mtumishi wa Idara ya Ardhi na Mipango Miji
kwa kosa la kujipatia fedha kinyume na taratibu za utumishi wa umma.
Akizungumza
leo mjini Bunda wakati wa tukio hilo, Bibi. Mayanja alisema kuwa
ameamua kumsimamisha kazi kwa muda, Bw.Eliudi Haonga ambaye ni mtumishi
wa Idara ya Ardhi na Mipango Miji pia ni Mthamini wa Halmashauri hiyo
ili kupisha uchunguzi kwa kosa la kujipatia fedha kinyume na taratibu
za utumishi wa umma.
“Tarehe
28 mwezi Juni mwaka huu Bw.Eliudi Haonga alipokea fedha kiasi cha
shilingi milioni saba kutoka kiwanda cha Olam ikiwa ni kodi ya pango
kwa mwaka kodi 2015/2016, lakini mtumishi huyo alihifadhi kwenye
akaunti ya Halmashauri ya mji yaani ‘own source’ fedha kiasi cha
shilingi milioni mbili tu, na kiasi kilichobaki yaani milioni tano
alizitumia kwa masuala binafsi kinyume na taratibu za utumishi wa umma”
alisema Bibi Mayanja
Aliongeza
kuwa Bw. Haonga aligushi risiti ya Halmashauri ya Mji na ambayo
aliikabidhi katika kiwanda cha Olam baada ya kupokea fedha hizo.
Alisisitiza
kuwa mtumishi huyo amesimamishwa kazi kwa mujibu wa kifungu namba 38
(1) cha kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2003.
Aidha,
Bibi Mayanja amewaasa watumishi wa umma wanaofanyakazi katika
Halmashauri hiyo kuwa waadilifu kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu
za nchi. Vile vile ameonya kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa
kwa yeyote atakayekiuka.
0 comments:
Post a Comment