Home » » MKURUGENZI WA ILEJE HAJI MNASI ATAKA MWALIMU NYERERE AENZIWE KWA VITENDO

MKURUGENZI WA ILEJE HAJI MNASI ATAKA MWALIMU NYERERE AENZIWE KWA VITENDO



 Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi akiwa katika makumbusho ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipotembele hivi karibu na kujifunza mambo mbalimbali aliyowahi kuyafanya hayati baba wa taifa kwa ajili ya kuleta maendeleo ya nchi nzima
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi akiwa katika kaburi la marehem Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere


Na fredy mgunda,musoma.

VIONGOZI wa vyama vya Siasa wametakiwa kuiga kwa vitendo uzalendo na moyo wa kujitoa  aliokuwa nao Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai wake  ili kuliwezesha Taifa kupiga hatua kimaendeleo.


Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Bw. Haji Mnasi ambaye kitaaluma ni mwalimu mara baada  kutembelea Kaburi na Makumbusho ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere eneo la Mwitongo wilayani Butiama.


mimi kitaaluma ni mwalimu hivyo namuezi mwalimu kwa vitendo hata nilipokuwa afisa elimu iringa nilikuwa naingia darasani kufundi na sasa nitahakikisha nazilinda mali za taifa,nasisitiza uwajibika,uzalendo,uandilifu na nidhamu katika kulitumikia taifa la Tanzania kama unakumbuka mwalimu alikuwa anapenda kutumia neno (it can be done play your part) kila mtu atimizi majukumu yakeAmesema Mnasi.



Amesema kuwa kumbukumbu za Baba wa Taifa zilizohifadhiwa vizuri katika makumbusho hiyo zina mambo mengi ya kujifunza ambayo wanasiasa wanatakiwa kuyafanya kwa  vitendo hasa  uzalendo kwa nchi, uvumilivu, upendo  na moyo wa kujitoa kwa dhati kuwatumikia wananchi.



“Kupitia kumbukumbu hizi sisi watumishi tumejifunza ukomavu wa demokrasia aliokuwa nao Mwalimu Nyerere akiwa ndani na nje ya Bara la Afrika,  wengi wanadhani Demokrasia ni wakati wa uchaguzi tu, kumbe demokrasia ni pamoja na kuheshimu watu wengine” Amesema Mnasi.



Ameeleza kuwa maisha aliyoishi Baba wa Taifa ni mfano wa kuigwa na viongozi na watanzania wote hasa pale alipojitofautisha na viongozi wengi wa Bara la Afrika alipoepuka tamaa ya madaraka na mali kwa  manufaa ya taifa.



“Sote ni mashahidi kupitia kumbukumbu zake tumeona mahali alipokuwa anaishi mwalimu kabla hajajengewa nyumba na Jeshi  kama Rais mstaafu wengi walitegemea asingeishi katika  eneo lile, kumbukumbu hii nzuri aliyoiacha inatufundisha watanzania kuwa mwalimu aliitanguliza Tanzania mbele kuliko maslahi yake binafsi” Amesisitiza Mnasi.



Bw. Mnasi amebainisha kuwa  serikali itaendelea  kumuemzi Baba wa Taifa kwa yale aliyoyafanya na kuyasimamia kwa manufaa ya taifa huku akitoa wito kwa  viongozi wa vyama vya Siasa wawe na kiasi na waridhike na vile walivyonavyo.



“Suala la kuridhika na kuwa na kiasi linapaswa kuzingatiwa, wanasiasa  wanapaswa kuwaheshimu wananchi wanaowachagua kupitia chaguzi mbalimbali,  matokeo yanapotoka kama ni sahihi basi wanasiasa wakubaliane na maamuzi yao”  Ameainisha Mnasi.

Bw. Mnasi amemalizia kwa kuwataka watendaji wote wa serikali ya wilaya ya Ileje kufanya kazi kwa uaminifu,uadilifu,kuwajibika kwenye majukumu yao na kujituma na kamwe hata kuwa tayari kuwavumilia watendaji ambao ni wazembe kazini.



Kwa upande wake Mhifadhi wa Makumbusho ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Bw. Jacob Thomas amesema kuwa  watanzania wanayo mengi ya kujifunza kupitia vitu alivyoviacha Baba wa Taifa ambavyo vimehifadhiwa katika Makumbusho hiyo.



Amesema kuwa maisha ya uadilifu aliyoishi enzi za uhai wake na mchango wake katika kuiletea maendeleo Tanzania na Bara la Afrika vinapaswa kuenziwa kwa nguvu zote na viongozi wa Tanzania.



“Ninyi mliopata nafasi ya kuitembelea makumbusho hii mmejifunza vitu vingi kumhusu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwamba alikuwa ni mtu wa namna gani kwa viwango vya Afrika na dunia kutokana na kumbukumbu ya uadilifu aliyoiacha ndani na nje ya mipaka ya Tanzania”


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa