NA DAUDI MANONGI, MAELEZO
DAR ES SALAAM.
UWEPO wa
kifungu kinachopendekeza uanzishwaji wa Baraza Huru la Habari katika Muswada wa
Huduma ya Habari wa mwaka 2016 utasaidia kukuza maadili na viwango vya taaluma
baina ya wanahabari na Kampuni za habari nchini.
Maoni hayo
yametolewa na Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dk Jim James
Yonazi leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hizi
Ameongeza kuwa
chombo hicho ni umuhimu kusimamia maadili ya Taalum ya habari na kufanya
waandishi wa habari hapa nchini wawajibike kwa kazi zao za kila siku za
kuhabarisha umma.
Mhariri huyo
Mtendaji amewahasa wanahabari kuukubali muswada unaopendekezwa kwani ni kwa
maslahi yao wenyewe na utaipa heshima taaluma hii.
“Sheria hii ni
muhimu sana kwa kuwa ukiangalia katika sekta zingine kama za
Uhasibu, Uhandisi ,wakandarasi na wanasheria wanatambuana kupitia vyombo ambavyo
wamejiwekea wakati sekta ya Habari
hakuna kitu kama hicho kinachoweza kuonyesha huyu ni mwanahabari na hata
kufahamu idadi yao nchini ni ngumu hata kuiendeleza katika viwango vya juu
uwezekano huo haupo”alisema Dk Yonazi.
Aidha
amewataka wamiliki na wadau wa tasnia ya Habari kuangalia mapungufu yake na kuona
ni wapi panatakiwa kuboreshwa na kusisitiza ni vema kuwa na sheria hii kwanza halafu
mapungufu yatafanyiwa kazi baadaye.
Kwa upande
mwingine amewataka wandishi kutokuwa waoga wa muswada huu na kutoa maoni yao
kama wafanyavyo katika mambo mengine na kuwataka kwa sasa kuruhusu utekelezaji
wa muswada huu na kuendelea kuusimamia na kuufatilia ili kujua wapi kuna tatizo
na kuliweka wazi ili liweze kurekebishwa.
Aidha
ameongeza kuwa muswada huo unakusudia kuanzisha Bodi ya Ithibati ya wanahabari ambayo
itasaidia katika kuwatambua waandishi wasio
wanahabari ambao wanachafua taaalum ya habari.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment