Disemba
19 hadi 25 mwaka huu, Mchungaji Josephine Miller (wa tatu kushoto)
kutoka Marekani alikuwa akifundisha na kuhubiri katika Kanisa la EAGT
Lumala Mpya Jijini Mwanza.
Baada
ya huduma hiyo, jana Disemba 27, wenyeji wake (pichani) wakiongozwa na
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola (wa sita
kulia) na Mama Mchungaji Mercy Kulola (wa tano kulia), walimtembeza
Mchungaji Miller katika hifadhi ya Taifa Serengeti ili kujionea vivutio
mbalimbali vilivyopo katika fidhahi hiyo.
Na BMG
Waumini wa EAGT Lumala Mpya wakifurahia uwepo wao ndani ya hifadhi
Mchungaji
Josephine Miller kutoka Marekani (kulia) akifurahia uwepo wake ndani ya
hifadhi ya Serengeti. Kushoto ni Mwanahabari na Blogger wa Lake Fm
Mwanza, George Binagi
Pundamilia, nyumbu na nyati wakiwa kwenye makundi ndani ya hifadhi ya Serengeti
Mama na Mwana
Twiga na upendo wao, hawaachani
Matukio yakiendelea kunaswa katika eneo la Viboko na Mamba
Tembo ndani ya hifadhi ya Serengeti
Simba mjamzito
Hili
ni daraja la waya ndani ya hifadhi ya Serengeti, ni katika eneo lenye
Viboko wengi. Kulia ni Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola akiwa na
Mwanahabari George Binagi
Mchungaji Josephine Miller akipanda daraja la kunesanesa, limetengenezwa kwa kama imara ya chuma Daraja la kunesanesa
Ni
muda wa chakula ndani ya hifadhi ya Serengeti huku pia Watalii wa Ndani
na Watalii wa Nje, wakifurahia pamoja uzuri wa hifadhi ya Serengeti.
Watanzania
wametakiwa kuongeza hamasa ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii
vilivyopo nchini ikiwemo hifadhi za Taifa ili kufurahia rasilimali
walizotunukiwa na Mwenyezi Mungu.
Mchungaji
Josephine Miller kutoka nchini Marekani aliyasema hayo jana wakati wa
ziara yake ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti ili kujionea
vivutio mbalimbali vya wanyama katika hifadhi hiyo.
Alisema
alipokuwa katika hifadhi mbalimbali barani Afrika ikiwemo za Afrika
Kusini na Zimbabwe, alikuwa akisikia kuhusu uzuri wa hifadhi ya
Serengeti hivyo amefurahia kutembelea hifadhi hiyo akisema kwamba hilo
lilikuwa ni chaguo lake la pili baada ya kuonana na watu wa bara la
Afrika.
Mchungaji
wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Kulola, alisema ni vyema
Mamlaka ya Hifadhi za Taifa TANAPA ikaongeza hamasa kwa Watanzania
kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kuukuza zaidi utalii
wa ndani huku akiomba suala la miundombinu ya barabara kuboreshwa ili
watalii.
Kumbuka
Mtanzania hulipa Tsh.11,800 pamoja na VAT kwa mtu mzima ili kuingia
katika hifadhi ya Serengeti. Wageni hulipa dolla 70 ikikadiliwa kuwa
Tsh, laki moja na elfu hamsini na nne. Hakika watanzania wanayo furusa
kubwa kutembelea vivutio vya vya utalii.
0 comments:
Post a Comment