Na
Hassan Silayo-MAELEZO
Wazee
wa Kimila kutoka Koo Tano Mkoani Mara wamemuomba Katibu Mkuu Wizara ya
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga kuwawezesha
kutembea Koo hadi Koo kwa ajili ya kuelimisha jamii kuhusu madhara ya
ukeketaji.
Akiongea
wakati walipokutana na Katibu Mkuu aliyepo Wilayani Tarime Mzee wa Koo ya
Bukenye Mzee Elias Maganya alisema kuwa walishapata elimu kutoka kwenye Jukwaa
la Kulinda Utu wa watoto(CDF) na changamoto ni jinsi ya kuzifikia koo nyingine
Mkoani huko ili kuwezesha kuondoa kabisa mila hiyo.
“Tumechoka
vitendo vya ukatili kwa watoto na vitendo visivyoturishisha sisi kama wazee,
tutafanya kila jitihada kuweza kuondokana na vitendo hivi, tunahitaji ushiriki
zaidi wa serikali na asasi nyingine zishirikiane na CDF ili kwa pamoja tuweze
kufikia lengo tuliloliweka” Alisema Mzee Elias
Akitolea
ufafanuzi suala hilo Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee
na Watoto Bi. Sihaba Nkinga amesema kweli upo umuhimu wa kutekeleza suala hilo
la kupeleka elimu juu ya madhara ya ukeketaji ili kuweza kuwasaidia watoto
wakike.
Naye
Mzee wa Kimila kutoka Koo ya Bukira Mzee Sinda Nyangore ameishauri serikali na
mashirika mengine kutoa elimu katika vipindi vyote vya mwaka na kuacha
utaratibu wa kutoa elimu katika msimu wa ukeketaji kwenye koo mbalimbali.
Katika
Ziara hiyo Katibu Mkuu Sihaba Nkinga alitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo
Dawati la Jinsia katika wilaya hiyo na kujionea namna wanavyofanya kazi na
jinsi wanavyokabiliana na changamoto mablimbali.
Aidha
Bi. Sihaba aliwatembelea watoto wa kike waliopo katika mpango wa uendelezwaji
kijasiriamali unaotekelezwa na Jukwaa la Kulinda Utu wa watoto(CDF) katika kata
ya Manga Wilayani Tarime Mkoani Mara.
0 comments:
Post a Comment