Takriban
mwezi mmoja tangu wachimbaji 15 wafukiwe na kifusi Nyarugusu wilayani
Geita, balaa jingine la aina hiyo limetokea wilayani Butiama mkoani
Mara.
Katika
tukio la Butiama, watu 11 wameokolewa shimoni wakichimba dhahabu na kwa
sasa wamelazwa Hospitali ya Wilaya ya Butiama kwa matibabu.
Mkasa
huo umetokea katika Mgodi wa Buhemba na Mkuu wa Wilaya ya Butiama,
Annarose Nyamubi amesema kazi ya uokoaji inaendelea kwa ajili ya
kuwatafuta watu wengine ambao ndugu zao hawajawaona na wanahisi
walikuwamo ndani ya shimo hilo.
Amesema mmomonyoko wa udongo ndiyo uliosababisha kuporomoka kwa mashimo hayo ya muda mrefu licha ya kuwapo jua kali.
Aidha
Nyamubi amesema mashimo hayo yaliyoachwa na mkoloni yako chini ya
mwekezaji StanCom ambaye ndiye aliyekuwa akichimba dhahabu katika eneo
hilo. Kufuatia tukio hilo, viongozi mbalimbali walifika kushuhudia
uokoaji akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dk Charles Mlingwa.
Chanzo: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment